ISRAELI-PALESTINA-HAMAS-Siasa-Usalama

Israel;Hadar Goldin ambaye anaaminika kutekwa na wapiganaji wa Hamas alifariki katika uwanja wa mapambano

Hadar Goldin ambaye anaaminika kutekwa na wapiganaji wa Hamas wakati wa mapambano
Hadar Goldin ambaye anaaminika kutekwa na wapiganaji wa Hamas wakati wa mapambano yahoo.com

Jeshi la Israel limesema askari wake aliyekuwa hajulikani alipo huko Gaza alipoteza maisha katika uwanja wa mapambano siku ya ijumaa.

Matangazo ya kibiashara

Hadar Goldin ambaye anaaminika kutekwa na wapiganaji wa hamas wakati wa mapambano na kusababisha kuvunjika kwa makubaliano ya usitishwaji wa mapambo maa baada ya israel kutoa tangazo la kupotea kwake.

Jeshi la Israel limesema limejiridhisha kuwa Luteni Goldin amepoteza maisha katika mapambano bila kufafanua kuwa linaushahidi wa maiti yake au la licha ya taarifa kudai jeshi hilo limefanya vipimo vya DNA na kujiridhisha.

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema operesheni ya kijeshi huko gaza itaendelea hadi usalama wa waisrael utakaporejea.

Kundi la Hamas limekanusha kumshikilia mateka askari huyo na kusema hamas haijui alipo askari huyo.