PALESTINA-ISRAELI-HAMAS-Usalama

Palestina: Gaza: Israeli na Hamas zakubaliana kusitisha mapigano

Raia wa Palestina katika mji wa Rafah, baada ya kupatikana kwa maiti ya mama yake katika vifusi vya nyumba iliyoteketezwa na sdhambulio la anga la jeshi la Israeli, jumatatu Ogasti 4 mwaka 20014.
Raia wa Palestina katika mji wa Rafah, baada ya kupatikana kwa maiti ya mama yake katika vifusi vya nyumba iliyoteketezwa na sdhambulio la anga la jeshi la Israeli, jumatatu Ogasti 4 mwaka 20014. REUTERS/Ibraheem Abu Mustafa

erikali ya Israeli na kundi la Hamas la nchini Palestina wamekubaliana kimsingi kutoa muda wa saa 72 kusitisha mapigano kwenye eneo la ukanda wa Gaza baada ya kuongezeka kwa shinikizo toka jumuiya ya kimataifa kuzitaka pande hizo kusitisha vita iliyodumu kwa siku 29 sasa.

Matangazo ya kibiashara

Makubaliano haya yamefikiwa mjini Cairo Misri, ikiwa ni siku tatu tu zimepita toka makubaliano ya awali ya kutoa siku tatu za kusitisha vita kushindikana kutokana na kila upande kuendelea na mapigano.

Marekani imepongeza uamuzi huo na kusisitiza kuwa ni kundi la Hamas pekee ndilo linalotakiwa kuheshimu makubaliano haya.

Makubaliano hayo yameanza kutekelezwa saa kumi na moja asubuhi saa za kimataifa. Makubaliano ya kusitisha mapigano ya saa 72 kati ya Israeli na Hamas ambayo yameanza kutekelezwa tangu asubuhi jumanne wiki hii, ni kufuatia mazungumzo kati ya pande husika na wajumbe kutoka mataifa mbalimbali yaliyofanyika katika mji mkuu wa Misri, Cairo.

Awali msemaji wa jeshi la Israeli, ametangaza kwamba wanajeshi wa Israeli wataondoka katika mji wa Gaza mapema humanne asubuhi wiki hii. “majeshi ya Israeli yataondoka katika mji wa Gaza na kujielekeza kwenye ngome zao, ambako wataimarisha ulizi”, amesema msemaji wa jeshi la Israeli.

Saa chache kabla ya utekelezaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano, afisa mmoja wa ngazi ya juu katika jeshi la Israeli, jenerali Moti Almoz, amethibitisha kwenye radio ya kijeshi kwamba, “wanajeshi wote wa Israeli wameondoka katika ukanda wa Gaza”.

wanajeshi wa Israeli wakijiandaa kuondoka katika mji wa Gaza, Jumanne Ogasti 5 mwaka 2014.
wanajeshi wa Israeli wakijiandaa kuondoka katika mji wa Gaza, Jumanne Ogasti 5 mwaka 2014. REUTERS/Baz Ratner

Milio ya risase imekua ikisikika mapema jumanne asubuhi pembezuni mwa mji wa Gazi. Huenda Uamzi huu wa Israeli kuondoa wanajeshi wake katika ukanda wa Gaza ni hatua ya kusitisha moja kwa moja mapigano.