ISRAEL-PALESTINA

Mapigano yarejea Gaza wakati huu jitihada za usitishwaji wa mapigano zikigonga mwamba

Athari ya mashambulizi ya anga yaliyofanywa na  Israel siku ya Jumamosi
Athari ya mashambulizi ya anga yaliyofanywa na Israel siku ya Jumamosi ©REUTERS/Ahmed Zakot

Ndege za kivita za Israel zimeripotiwa kufanya mashambulizi Gaza jumamosi ikiwa ni siku moja baada ya kuua takribani wapalestina watano na kushuhudia wapiganaji wa Hamas wakishambulia israe kwa maroketi baada ya kushindwa kwa jaribio la kuongeza siku tatu za usitishwaji wa mapigano.

Matangazo ya kibiashara

Mzozo huo uliodumu kwa mwezi sasa umerejea tena baada ya wapatanishi kushindwa jitihada za kuongeza muda wa usitishwaji wa mapigano.

Hata hivyo Marekani inamatumaini kuwa hali itarejea kuwa tulivu na usitishwaji wa mapigano utashughulikiwa katika kipindi kifupi.

Misri ambayo imekuwa mpatanishi wa Israel na Palestina imesisitiza kuwa majadiliano yalikuwa yakiendelea vema na kutaka pande hizo mbili kujadiliana makubaliano mapya huku Israel ikijibu kuwa haiwezi kufanya majadiliano wakati ikishambuliwa.

Waziri Mkuu wa Isarel Benjamin Netanyahu ameliamuru jeshi lake kujibu mashambulizi huku akilaumu kundi la Hamas kwa kukiuka maadili ya kusitisha mapigano.

Wanamgambo wa Palestina fwalifyatua makombora 40 wakishambulia Israeli, na kujeruhi raia mmoja na askari, jeshi la israel lilisema na kujibu mashambulizi likilenga maeneo 51 yanayokaliwa na magaidi huko Gaza.