PALESTINA-ISRAELI-HAMAS-Usalama

Gaza: Hamas na Israel wakubaliana kusitisha mapigano

KIfaru cha jeshi la Israeli kikipiga doria karibu na mapaka wa Gaza.
KIfaru cha jeshi la Israeli kikipiga doria karibu na mapaka wa Gaza. REUTERS/Amir Cohen

Muda mwingine wa saa 72 wa kusitisha vita katika ukanda wa gaza umeanza tena mapema asubuhi jumatatu wiki hii ambapo wajumbe katika majadiliano wanakutana kuhakikisha muda huu unakuwa wa kudumu na kusitishwa moja kwa moja kwa mapigano kati ya Israel na Kundi la Hamas yaliogharimu maisha ya watu takriban elfu mbili.

Matangazo ya kibiashara

Tawi ka kijeshi la kundi la Hamas Brigade Ezzedine Al Qassam imetangaza katika taarifa yake jana kwamba imerusha maroketi katika ardhi ya Israel huku moja ikianguka mjini Tel Aviv, saa chache kabla ya kuanza kutekelezwa kwa muda wa kusitishwa mapigano.

Jeshi la Israel limesema roketi iliorushwa katika mji wa Tel Aviv haijaathiri pakubwa makaazi ya wananchi.

Hapo jana Israel na Hamas wameafikiana baada ya mvutano wa muda mrefu kusitisha mapigano kwa muda mwingine wa saa 72 chini ya usuluhishi wa Misri.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amepongeza hatua hiyo ya kusitishwa kwa mapigano kwa muda wa saa 72 na kutowa wito kwa israel na Hamas kujadiliana kuhusu mpango wa kupatikana kwa muda mrefu wa kusitishwa vita.

Ban Ki Moon amesema kuna matumaini kwa pande hizo mbili chini ya usuluhishi wa Misri kupatikana kwa bahati nyingine ya kusitishwa vita kwa muda mrefu kwa manufaa ya wananchi na ni hatuwa ya kuanzia kwa Israel na Palestina kutowa malalamiko yao.

Israel na wajumbe wa Hamas wanaongoza katika ukanda wa Gaza pamopja na washirika wao wa Islamic Jihad na wale wa Fatah wanaendesha mazungumzo tangu kupindi kadhaa kuhakikisha muafaka wa kusitishwa vita kwa takriban siku 3 unapatikana.

Israel na Hamas zimetupiiana lawama, Israel yaituhumu Hamas kukiuka makubaliano, wakati Hamas ikiituhumu Israel kushindwa kutekeleza makubaliano ya kuondowa viziwizi katika Ukanda wa gaza.