ISRAELI-PALESTINA-CAIRO-HAMAS

Cairo : Palestina : makubaliano ya kusitisha mapigano moja kwa moja yajadiliwa

Ujumbe wa Palestina katika mazungumzo yanayofanyika mjini Cairo, nchini Misri.
Ujumbe wa Palestina katika mazungumzo yanayofanyika mjini Cairo, nchini Misri. REUTERS/Asmaa Waguih

Wakati zikisalia saa chache ili muda wa siku 5 wa makubaliano ya kusitisha mapigano ufikiye tamati, serikali ya Israel hapo jana jumapili imesisitiza kuwa haitakubaliana na mapendekzo yoyote ya kuongeza muda zaidi wa usitishwaji wa mapigano kwenye eneo la Ukanda wa gaza, iwapo nchi hiyo haitapewa hakikisho la usalama.

Matangazo ya kibiashara

Israel inatoa kauli hii wakati ambapo mazungumzo kuhusu usitishwaji wa makabiliano kwenye eneo la ukanda wa Gaza yakianza tena mjini Cairo, Misri wakati huu ambapo ule muda wa siku tano wa kusitisha mapigano ukitarajiwa kutamatika hii leo majira ya saa tatu usiku.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Jonh Kerry (kushoto) akiongea na waziri mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu (kulia) mjini Tel-Aviv kabla ya kujielekeza mjini Cairo kushiriki mazungumzo ya kusitisha mapigano..
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Jonh Kerry (kushoto) akiongea na waziri mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu (kulia) mjini Tel-Aviv kabla ya kujielekeza mjini Cairo kushiriki mazungumzo ya kusitisha mapigano.. REUTERS/Pool

Wakati huo huo waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amesisitiza kuwa wapatanishi wa nchi yake wanaoshiriki mazungumzo ya kusaka amani kati yake na Palestina mjini Cairo Misri, wanamaelekezo thabiti kuhusu nchi yao kuhakikishiwa usalama dhidi ya kundi la Hamas ndipo wakubali kuongeza muda wa kusitisha mapigano kwenye eneo hilo.

Katika hatua nyingine kiongozi wa ujumbe wa Palestina kwenye mazungumzo hayo, Azzam al-Ahmadi amesema yako matumaini ya pande hizo mbili kufikia suluhu.

Katibu mkuu wa jumuiya ya nchi za kiarabu, Nabil Elaraby akiwa pamoja na rais wa Mamlaka ya Palestina,Mahmoud Abbas katika jitihada za kupatia ufumbuzi mapigano kati ya Israeli na Hamas katika ukanda wa Gaza.
Katibu mkuu wa jumuiya ya nchi za kiarabu, Nabil Elaraby akiwa pamoja na rais wa Mamlaka ya Palestina,Mahmoud Abbas katika jitihada za kupatia ufumbuzi mapigano kati ya Israeli na Hamas katika ukanda wa Gaza. REUTERS/Asmaa Waguih

Wakati huo huo wafadhili wa kimataifa kwa ajili ya Palestina wanakutana jumatatu wiki hii mjini cairo kwa lengo la kufadhili ujenzi katika ukanda wa Gaza, iwapo mkataba wa kusitisha mapigano utakua umetekelezwa kati ya Israel na palestina, Norway imetibitisha jumatatu wiki hii.

Pesa zitakazokusanywa chini ya kivuli cha Misri na Norway zitakabidhiwa rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas, amesema waziri wa Norway mwenye dhamana ya mambo ya nje, Boerge Brende, ambaye nchi yake inaongoza kamati ya kuratibu misaada ya kimataifa kwa raia wa Palestina.

Hayo yakijiri, wizara ya afya ya palestina imethibitisha jumatatu wiki hii kwamba wapalestina 2016 wameuawa katika mashambulizi yaliyotekelzwa katika ukanda wa Gaza tangu mwanzoni mwa mwezi Julai na jeshi la Israeli.

Kwa mujibu wa wizara hiyo, miongoni mwa wapalestina 2016 waliouawa, 541 ni watoto na 250 ni wanawake.