Dola la Kiislam: jumuiya ya nchi za kiarabu inaunga mko fikra ya ushirikiano wa kimataifa
Imechapishwa:
Mawaziri wa mataifa ya kiarabu wamekubaliana jumapili Sptemba 7 mjini cairo, nchini Misri kuchukua hatua zinazohitajilia kwa kukabiliana na Dola la kiislam pamoja na kutoa ushirikiano wao katika juhudi za kimataifa, kikanda au kitaifa kwa kupambana na makundi ya kiislam yenye silaha.
Katika kikao hicho mawaziri hao wamekuabaliana kusitisha misaada ya kijeshi hususana sialaha na vifaa vingine vya jeshi pamoja na fedha kwa makundi ya kiislam yenye silaha nchini Iraq na Syria.
Azimio la jumuiya ya nchi za kiarabu ni kujilinda kwa mataifa wanachama wa jumuiya hiyo dhidi ya vitisho vya Dola la Kiislamu pamoja na makundi mengine ya kiislam ya kugaidi katika ulimwengu wa kiarabu.
“ Hatutokubali kuendelea kwa vitisho hivyo ya Dola la Kiislamu”, amesema katibu wa jumuiya ya nchi za kiarabu, Nabil Al Arabi.
Kuongezeka kwa makundi ya wapiganaji wa kiislamu wenye msimamoamo mkali imekua ni tishio kwa mataifa wanachama wa jumuiya ya nchi za kiarabu, hadi kupelekea baadhi ya mataifa hayo kuvunja ushirikiano wao na makundi hayo.
Azimio la jumuiya ya nchi za kiarabu linatoa fursa kwa taifa lolote mwanachama wa jumuiya hiyo kutoa ushiriki wake kwa Marekani ambayo imekua ikitoa wito kwa mataifa kushirikiana kwa pamoja dhidi ya Dola la Kiislam.
Waziri wa Marekani mwenye dhamana ya mambo ya nje, John Kerry, aliongea hivi karibu na katibu wa jumuiya ya nchi za kiarabu, Nabil Al Arabi kuhusu uwezekano huo wa kushirikiana kwa pamoja dhidi ya Dola la Kiislamu.