Ushirikiano dhidi ya Dola la Kiislam: mataifa ya Ghuba yakutana
Imechapishwa:
Barack Obama alitangaza hivi karibuni kwamba atahakikisha amelisambaratisha Dola la Kiislam ikiwa nchini Iraq au Syria, baada ya Marekani kuuungwa mkono na Saudia Arabia, moja ya mataifa ya kiarabu.
Mchakao ambao umeanzishwa na Marekani ni kushawishi mataifa mengine ya kiarabu kutoa ushiriki wao katika vita hivyo. Hiyo ni moja ya agenda ya mazungumzo yanayowakutanisha alhamisi wiki hii viongozi wa mataifa ya kiarabu katika mji wa Djeddah nchini Saudia Arabia.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry atakutana na wenzaki kutoka mataifa ya Ghuba, lakini pia atakutana na mawaziri wa mambo ya nje wa Jordan, Misri, Uturuki na Liban. Swali ni kujua iwapo mataifa yote hayo yanaunga mkono kushambuliwa kwa Dola la Kiislam.
Baada ya kukubali kutoa nafasi ya mafunzo kwa waasi wa Syria, Saudia Arabia ina mchango mkubwa kwa kuyashawishi matiafa mengine ya kiarabu kuunga mkono mashambulizi dhidi ya Dola la Kiislam. Hayo ni baada ya kujitokeza mvutano kati ya Doha, Riyadh na Abou Dhabi kuhusu vita hivyo.
Qatar imekua ikishukiwa kufadhili na mataifa jirani pamoja na mataifa ya magharibi kwamba imekua ikifadhili makundi ya kiislam. Rais wa Marekani, Barack Obama katika hotuba yake ya hivi karibuni, alikemea tabia hiyo ya Qatar.
Marekani imekua ikitaka kuyashirikisha mataifa yote Ghoba ili yaunge mkono mpango wake wa kushirikiana kwa kupambana na wapiganaji wa Dola la Kiislam.