ISRAELI-PALESTINA-HAMAS

Israel: maafisa na wanajeshi 40 wajiuzulu

Kikosi cha wanajeshi wa ardhini cha Israel katika ukanda wa Gaza, Julai 12 mwaka 2014.
Kikosi cha wanajeshi wa ardhini cha Israel katika ukanda wa Gaza, Julai 12 mwaka 2014. REUTERS/Finbarr O'Reilly

Maafisa arobaini wa jeshi na wanajeshi wa ziada, ambao wanaunda kitengo maalumu cha ujasusi wa kijeshi chini Israel wameamua kujiuzulu, wakikataa kuendelea kutumiwa kwa kutekeleza vitendo viovu dhidi ya wapalestina.

Matangazo ya kibiashara

Hayo yamo katika barua maafisa na wanajeshi hao waliyoandika ambayo ilichapishwa ijumaa katika vyombo vya habari.

Gazeti la Yediot Aharanot linalosomwa na watu wengi, limechapicha hivi karibuni sehemu ya barua hiyo. Ikiwa barua hiyo ni sahihi, itakua ni moja ya maamuzi muhimu yanayochukuliwa na raia wa Israel dhidi ya msimamo wa serikali tangu miaka kadhaa iliyopita.

Wanajeshi hao wanawake na wanaume, waliyosaini kwenye barua hiyo walihudumu katika kitengo cha ujasusi wa jeshi cha 8200, gazeti la Yediot Aharanot limeeleza.

Kitengo hicho ambacho kinalinganishwa na Shirika la kitaifa la Usalama nchini Marekani NSA, kina uzowefu katika masuala ya ulinzi kupitia intaneti. Wanajeshi hao wa ziada wanaweza kuitishwa mahakamani kwa muda wowote.

Hata hivo wanajeshi hao 43, ambao majina yao hayakutajwa katika vyombo vya habari, wamekataa kata kata kuendelea kuhudumu katika kitengo hicho, ambacho wanadai kwamba kimekua kikihatarisha usalama wa mamilioni ya raia.

Barua hiyo walioandika imewasilishwa kwa waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, na kwa mkuu wa majeshi.

Hakuna ushahidi wa wanajeshi hao waliyokataa kuendelea kuhudumia jeshi la Israel, ambao unaonesha kuwa uamzi waliochukua unaambatana na mashambulizi ya jeshi la Israel yaliyoendeshwa mwezi Julai na Agosti katika ukanda wa Gaza.

Jeshi la Israeli likiendesha mashambulizi ya anga katika ukanda wa Gaza.
Jeshi la Israeli likiendesha mashambulizi ya anga katika ukanda wa Gaza. (Photo : Reuters)

Mwanamke mmoja miongoni mwa wanajeshi hao amebaini kosa kubwa alilofanya lilosababisha kifo cha mtoto mchanga. Wengine wameelezea masikitiko yao kuona walitumiwa kwa kipindi kirefu kwa kusikiliza kwa simu mazungumzo ya wapalestina ambayo hayakua hata yanawahusu.

“ Tunatolea wito wanajeshi wote ambao wanaendelea kuhudumu aidha watakao hudumu katika kitengo hicho pamoja na wananchi wa Israel kupaza sauti zao dhidi ya maovu hayo yanayotendewa wapalestina ili yaweze kukomeshwa”, wameeleza katika barua yao.

Wanajeshi hao 43 wanakabiliwa na adhabu ya kifungo jela.