PALESTINA-ISRAELI-Usalama

Palestina: raia wanaotuhumiwa mauwaji ya wasichana 3 wa Israel wauawa

Mabaki ya nyumba ya Hussam Qawasmeh, mmoja wa washukiwa wa mauaji ya vijana wa kiisrael, waliotekwa nyara na baadae kuuawa katika mji wa Cisjordania.
Mabaki ya nyumba ya Hussam Qawasmeh, mmoja wa washukiwa wa mauaji ya vijana wa kiisrael, waliotekwa nyara na baadae kuuawa katika mji wa Cisjordania. AFP PHOTO/ HAZEM BADER

Raia wa Palestina wanaotuhumiwa kuwateka nyara na kuwaua vijana wa Israel mwezi Juni mwaka huu, wameuawa katika operesheni iliyoendeshwa mapemajumanne asubuhi wiki hii katika mji wa Cisjordania.

Matangazo ya kibiashara

Watu hao wamekua wakitafutwa kwa muda wa miezi mitatu sasa. Hayo yanajiri wakati mazungumzo kati ya Israel na Palestina yanatazamiwa kuanza jumanne wiki hii nchini Misri.

Operesheni hiyo imeendeshwa usiku wa jumatatu kuamkia jumanne katika mji walikokua wakiishi watuhumiwa hao wawili: Marwan Qawasmeh na Amer Abou Eisheh. Jeshi la Israel limejizuia kutoa taarifa zaidi lakini gazeti la serikali Haaretz limesema kuwa operesheni hiyo iliendeshwa kwa muda mfupi lakini likua ngumu. Baadhi ya watu wamekamatwa katika operesneni hiyo.

Ni miezi mitatu sasa Marwan Qawasmeh na Amer Abou Eisheh wamekua wakisakwa, wakituhumiwa kuwateka na kuwaua vijana watatu wa kiisrael karibu na eneo la walowezi wa kiisrael katika mji wa Cisjordania. Watu hao wameklua wakituhumiwa kwamba walitekeleza kitendo hicho kwa amri ya Hamas.

Awali familia za watuhumiwa hao zilikanusha kuhusika kwa watu hao katika kuwateka na kuaua vijana hao wa kipalestina. Mtu mwengine,a mbaye anajulikana kwa jina la Hussam Qawasmeha alikamatwa hivi karibuni na kutuhumiwa kwamba alifadhili na kuandaa mauaji hayo.