MAREKANI

Jeshi la Marekani: Tunadhoofisha Islamic State nchini Syria

Ndege za kivita zikishambulia ngome za Islamic State
Ndege za kivita zikishambulia ngome za Islamic State REUTERS/U.S. Air Force

Jeshi la Marekani linasema mashambulizi ya angaa dhidi ya wapiganaji wa Kiislamu wa Islamic State nchini Syria yanadhoofisha wapiganaji hao baada ya vituo vya mafuta walivyokuwa wanadhibiti kuteketezwa.

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo, Mkuu wa Majeshi Jenerali Martin Dempsey amesema mashambulizi ya angaa pekee hayawezi kutegemewa kuwamaliza kabisa wapiganaji hao nchini Syria na Iraq.

Aidha, Jenerali Dempsey amesema suluhu la kisiasa linahitajika nchini Iraq na Syria ili kupata amani ya muda mrefu katika nchi hizo mbili.

Siku ya Ijumaa, wabunge nchini Uingereza nao walikubali jeshi lao kujiunga na Marekani, Ufaransa na mataifa mengine ya Ulaya na kutoka Umoja wa Kiarabu kuwashambulia wapiganaji hao.

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Chuck Hagel (Kushoto) akiwa na Mkuu wa Majeshi Jenerali Martin Dempsey (Kulia)
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Chuck Hagel (Kushoto) akiwa na Mkuu wa Majeshi Jenerali Martin Dempsey (Kulia)

Katika hatua nyingine, Marekani inasema wapiganaji wa jeshi huru la Syria linahitajika kupambana na wapiganaji hao wa Islamic State ardhini ili kudhibiti kabisa ngome za wapiganaji hao.

Zaidi ya Mataifa 40 yamejiunga na Marekani kuongoza mashambulizi dhidi ya wapiganaji hao ambao wanaedelea kusababisha mauaji ya raia na kuchukua maeneo zaidi.

Mwanajeshi wa Iraq
Mwanajeshi wa Iraq REUTERS/Alaa Al-Marjani

Siku ya Ijumaa, Waziri wa Mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov alishtumu mashamabulizi ya angaa nchini Syria bila ya kuishirikisha Moscow.