YEMEN-Usalama

Yemen: shambulio la kigaidi lagharibu maisha ya watu

Mmoja kati ya majeruhi aondolea katika eneo la tukio katika mji wa Sanaa, nchini Yemen, Oktoba 9 mwaka 2014.
Mmoja kati ya majeruhi aondolea katika eneo la tukio katika mji wa Sanaa, nchini Yemen, Oktoba 9 mwaka 2014. REUTERS/Khaled Abdullah

Watu 43 wameuawa mapema leo Alhamisi asubuhi katika shambulio la kigaidi katika mji mkuu wa Yemen, Sanaa. Shambulio hilo limekua limewalenga waandamanaji ambao ni watu kutoka dhehebu la Washia kufuatia machafuko ya kisiasa yanayoendelea kushuhudiwa nchini Yemen.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa mashahidi, shambulio hilo limetokea katikati ya mji mkuu wa Yemen, Sanaa, wakati wafuasi wa waasi wa kishia wamekua wakijiandaa kuandamana kama wanavyofanya kila siku kwa majuma kadhaa sasa. Raia hao wakishirikiana na waasi wa kishia waliandamana hadi kuudhibiti mji wa Sanaa Septemba 21.

Kwa sasa Yemen inakabiliwa na hali ya sintofahamu, hususan maandamano yanayoendeshwa na raia wachache kundi la Houth, linaloongozwa na Abdelnalek Al Houth, liliomba hivi karibuni kujiuzulu kwa mawaziri wawili kwenye wadhifa wa Waziri mkuu, ombi ambalo lilitekelezwa na mawaziri hao. Waziri wa pili aliye teuliwa kwenye wadhifa wa Waziri mkuu Jumanne wiki hii alijiuzulu jana Jumatano kufuatia shinikizo la waasi wa kishia.

Kwa miaka kadha Yemen imekua ikishuhudia mashambulizi yaliyokua yakitekelezwa na kundi la Aqpa, lenye mafungamano na kundi la Al qaeda, ambalo limeahidi kupambana dhidi ya waasi wa kishia. Hakuna kundi ambalo limekiri kuhusika na shambulio liliyotokea Alhamisi wiki hii, lakini kuna uwezekano wa kuambatanisha tishio hilo na shambulio la leo Alhamisi.

Yemen inakabiliwa na maandamano yalioanza tangu mwaka 2011, huku mapigano yakishuhudiwa kati ya watu kutoka madhehebu mawili (Washia na Wasuni).