Pata taarifa kuu
LIBAN-Al Nosra-Mapigano-Usalama

Libanon: mapigano yaendelea kurindima Tripoli

REUTERS/Omar IbrahimREUTERS/Omar Ibrahim
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Maelfu ya raia waliendelea kulikimbia Jumapili jioni Oktoba 26 eneo moja la mji wa Tripoli, mji mkubwa wa Libanon, ambao unakabiliwa na mapigano kwa muda wa siku tatu sasa.

Matangazo ya kibiashara

eshi la Libanon limeendelea kuendesha mashambulizi katika eneo moja linalokaliwa na wapiganaji wa kiislam. Wanajeshi wanne wameuawa.

Wakati huo huo, kundi la Al-Nosra lenye mafungamano na kundi la Al Qaeda limeendelea na vitisho vya kumuua mmoja kati ya wanajeshi linaowashikilia tangu mwezi Agosti katika mji wa Ersal, karibu na mpaka wa Syria.

Kufuatia mapigano yanayoendelea katika mji wa Tripoli kwa siku ya tatu mfululizo, jeshi la Libanon limetenga eneo watakalopitia raia wanao kimbia mapigano katika kata ya Bab al-Tebbaneh.

Watu wanaoyakimbia mapigano hayo wamekua wakipokelewa na wahisani wa shirika la msalaba mwekundu, ambao wamekua wakiwapeleka katika maeneo salama au katika shule ziliyotengewa kwa mapokezi ya wakimbizi hao.

Katika mji wa Saïda, kusini mwa Beyrut, idadi ya wanajeshi imeongezwa. Wanajeshi wametumwa pembezuni mwa kambi ya wakimbizi wa Kipalestina ya Aïn el-Héloué, ambapo baadi ya maeneo yanakaliwa na wapiganaji wa kiislam.

Viongozi wa Libanon wamebaini kwamba vita hivyo vitachukua muda mrefu.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.