ISRAELI-PALESTINA-Siasa-Usalama

Netanyahu aapa kuendelea na mpango wa ujenzi wa nyumba 1000 Jerusalem

Waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu.
Waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu. Reuters/Debbie Hill/Pool

Waziri Mkuu wa Israeli Benjemin Netanyahu ameshtumu Mataifa ya kigeni yanayopinga mpango wa serikali yake kujenga makaazi zaidi ya elfu moja Mashariki mwa Mji wa Jerusalem.

Matangazo ya kibiashara

Netanyahu amekanusha kuwa ujenzi wa makaazi hayo ya Kiyahudi yanarudisha nyuma juhudi za upatikanaji wa amani kati ya Israeli na Palestina na kusisitiza kuwa wanaosema hivyo hawafahamu ukweli.

Tayari Palestina imeonya kuwa ikiwa ujenzi huo utaendelea, utazua machafuko kati yake na Isreal kama iliyovyokuwa mweiz wa nane mwaka huu.

Netanyahu amesisitiza kuwa licha ya ukosolewaji mkubwa kutoka kwa Mataifa ya Ulaya na Marekani, ujenzi huo utaendelea kama ilivyopangwa.

Uamzi huo wa Israeli ni kinyume na sheria za kimataifa, na unakuja wakati ambapo mji huo wa jerusalem unaendelea kushuhudia hali ya machafuko.

Israeli imeongeza pia kuwa, makaazi mengine yatajengwa katika ukingo wa Magharibi kutumiwa na Waisraeli na Wapelestina.

Jibril Rajoub, mshirika wa karibu wa rais wa Palestina Mahmud Abbas amesema ujenzi huo mpya huenda ukasababisha vita.

Israeli imekuwa ikisisitiza kuwa haiwezi kuiachia mji wa Jerusalem kutokana na sababu za kihistoria, dini na usalama, lakini Palestina inasema Mashariki mwa mji huo ni sehemu yake.

Wakaazi wa mji wa beit Hanina wameelezea kukerwa na uchokozi wa Israeli wa kuanzisha ujenzi katika maeneo ambayo si milki yake.