Jerusalem-Israeli- Palestina-Usalama

Machafuko yaendelea kushuhudiwa kati ya Israel na Palestina

Tangu kutokea kwa mashambulizi mfululizo katika wiki za hivi karibuni katika mji wa Jerusalem, usalama umeimarishwa.
Tangu kutokea kwa mashambulizi mfululizo katika wiki za hivi karibuni katika mji wa Jerusalem, usalama umeimarishwa. REUTERS/Ammar Awad

Mashambulizi mawili kwa kutumia kisu yametokea Jumatatu Novemba 10 karibu na makaazi ya walowezi wa Kiyahudi katika miji ya Cisjordania na Tel Aviv, na kusababisha vifo vya watu wawili ikiwa ni pamoja na mwanajeshi na msichana.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa polisi, mashambulizi hayo yametekelezwa na raia wawili wa Palestina, ambao mmoja aliuawa na mwengine amekamatwa. Mashambulizi hayo yanatokea baada ya mashambulizi mengine mfululizo kushuhudiwa wiki iliyopita katika mji wa Jerusalem Mashariki. Hali hii imeanza kuwatia wasiwasi raia wa Israeli.

Shughuli zimendelea kama kawaida Jumatatu alaasiri Novemba 10 katika mji wa Jerusalem, licha ya kuwa wakaazi wa mji huo ambao wengi wao ni raia wa Israeli wamekua na wasiwasi ya kutokea kwa wakati wowote mashambulizi mingine.

Wakati huohuo, baadhi ya vijana wa Kiisraeli wamesema hawatokubali hali hiyo iendelee, bali wataamua kujiunga na jeshi ili kukomesha vitendo hivyo vya kigaidi.

Noa, msichana mwenye umri wa miaka 18 hafichi hisia zake: “ Mwanajeshi mmoja amelengwa na moja kati ya mashambulizi yaliyotokea katika mji wa Tel Aviv. Nina marafiki katika jeshi, hata mimi nitajiunga na jeshi mnamo miezi miwili ijayo. Naona kuwa usalama wangu uko hatarini, ninaweza kushambuliwa wakati wowote. Nina wasiwasi na hali hii”, amesema Noa.

Viongozi wa Israel wameimarisha usalama. Wanajeshi na askari polisi wameanza kupiga doria katika mitaa mbalimbali ya mji wa Jerusalem Mashariki.