ISRAELI-PALESTINA-JERUSALEM-Siasa-Usalama

Israeli yaruhusu ujenzi wa nyumba 78 katika ardhi ya Palestina

Wanawake wa Palestina pamoja na Askari polisi wa Israeli, kila upande ukiangalia mwengine, katika eneo la Jabal Al Mkaber, Jerusalem, Novemba 18 mwaka 2014.
Wanawake wa Palestina pamoja na Askari polisi wa Israeli, kila upande ukiangalia mwengine, katika eneo la Jabal Al Mkaber, Jerusalem, Novemba 18 mwaka 2014.

Waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu ameruhusu ujenzi wa nyumba 78 katika maeneo yanayokaliwa na walowezi katika ardhi ya Palestina.

Matangazo ya kibiashara

Uamzi huo wa Netanyahu unakuja wakati ambapo hali ya wasiwasi imeendelea kutanda katika maeneo mbalimbali ya miji ya Jerusalem Mashariki na Jerusalem Magharibi.

Tangu vijana wawili wa Kipalestina watekeleze shambulio dhidi ya Sinagogi Jumanne Novemba 18 katika mji wa Jerusalem, raia wa Israeli na Palestina wameendelea kuwa na wasiwasi. Raia wa Israeli wana hofu ya kutokea kwa mashambulizi mapya, huku raia wa Palestina wakihofiwa kwamba Israeli huenda ikajilipiza kisase kufuatia mashambulizi ya hivi karibuni dhidi ya Sinagogi mjini Jerusalem.

Askari polisi wa Israeli wamezuia barabara zinazoingia na kutoka katika eneo la Jabal Al-Mukaber, eneo la mji wa Jerusalem linaokaliwa na Warabu. Raia wawili wa Palestina walioendesha shambulio dhidi ya Sinagogi wanaishi katika eneo hilo.

Raia wa eneo hilo la Jabal-Al-Mukaber liliyo karibu na eneo linalokaliwa na wayahudi, wanahofu ya kushambuliwa na raia wa Israeli.

“ Tuna hofu ya kushambuliwa, kwa sababu, walowezi wote wanamiliki silaha”, amesema Hanin, mvulana wa Kiarabu, mwenye umri wa miaka 13.

Katika eneo hilo la Jabar Al-Mukaber, raia wa Palestina wanakabiliana mara kwa mara na polisi ya Israeli. Lakini tangu kutikee shambulio dhidi ya Sinagogi, ushirikiano kati ya Waisraeli na Warabu umeendelea kudorora.