ISREALI-PALESTINA-Usalama-Siasa

Israel: Serikali yapitisha muswada wa sheria kuhusu taifa la Wayahudi

Serikali ya Benyamin Netanyahu imepitisha jumapili Novemba 23 muswada unaotambua Israel kama taifa la Wayahudi.
Serikali ya Benyamin Netanyahu imepitisha jumapili Novemba 23 muswada unaotambua Israel kama taifa la Wayahudi. REUTER/Baz Ratner

Wakati mzozo kati ya Israel na Palestina ukiendelea kufukuta, Serikali ya Israel imepitisha muswada wa sheria unaolitambua eneo la Jerusalem kama ardhi rasmi ya walowezi wa Kiyahudi.

Matangazo ya kibiashara

Mapendekezo haya ya Sheria sio tu yanalitambua taifa hilo kama taifa la kiyahudi na demokrasia lakini kwenye muswada huu mpya unalitambua kwa ujumla kama taifa la kiyahudi, hatua itakayoshuhudia kutengwa kwa watu zaidi ya milioni 1 na laki saba ambao wana asili ya kiarabu.

Vyama vya upinzani kikiwemo kile cha waziri wa sheria Zipi Livn na waziri wa fedha Yesh Atid walipiga kura ya hapana wakati wa uidhinishwaji wa mapendekezo ya muswada huo wa sheria waliodai utazidi kuchochea mzozo kwenye eneo la ukingo wa magharibi.

Wachambuzi wa mambo wanaona kuwa muswada huu umelenga kuondoa sura ya kidemokrasia iliyokuwa inatambulika na taifa hilo na badala yake imelenga utaifa wa watu wa kiyahudi ambao ndio wengi.

Wataalamu wa taasisi ya demokrasia nchini humo wamesema kuwa muswada huu wa sheria sio jambo jipya kwa kuwa taifa la kiyahudi linatambulika hata kwenye mkataba wa uhuru wa nchi hiyo wa mwaka 1948.