SYRIA-LEBANON-UN-WFP-Wakimbizi-Misaada

Wakimbizi wa Syria: wito wa kusaidia Lebanon

Katika kambi ya wakimbizi ya Bekaa. Lebanon inapokea wakimbizi wengi duniani.
Katika kambi ya wakimbizi ya Bekaa. Lebanon inapokea wakimbizi wengi duniani. REUTERS/Mohamed Azakir

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limesitisha msaada wa chakula kwa wakimbizi wa Syria. Shirika hilo la Umoja wa Mataifa linakabilia na ukosefu wa fedha ili kufadhili programu yake.

Matangazo ya kibiashara

Kwa jumla, wakimbizi milioni 1.7 watakosa msaada wa chakula kwa mwezi huu wa Desemba katika nchi za Jordan, Uturuki, Iraq, Misri, lakini pia Lebanon, nchi za ukanda huo ambazo zimekua zikipokea idadi kubwa ya wakimbizi wa ndani. Zaidi ya wakimbizi milioni 1.1 wamesajiliwa na Umoja wa Mataifa.

Uamzi huo wa Umoja wa Mataifa wa kusitisha misaada ya chakula kwa wakimbizi wa Syria utakuwa na athari kubwa kwa nchi ya Lebanon, ambayo tayari ina matatizo mengi ya kurasibu suala hili. Kwa zaidi ya raia wa Syria milioni 1.1 ambao wameorodheshwa na Umoja wa Mataifa, sawa na robo ya wakazi wake. Hata hivyo Lebanon ni nchi ambayo inapokea wakimbizi wengi duniani.

Lebanon kwa sasa inakabiliwa na wingi wa wakimbizi, na hali hiyo inahatarisha uchumi wakei. Idara za kijamii ziko chini ya shinikizo, huku sekta ya afya, elimu na miundombinu zikiathirika, bila kusahau mdororo wa usalama.

Bila misaada ya kimataifa, Lebanon itashindwa kuhudumia raia hao wasiojiweza. Kufuatia hali hii, viongozi wa Lebanon wametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kusaidia raia hao, ikibainisha kwamba nchi hiyo inakabiliwa na mataizombalmbali, hususan mdororo wa uchumi.