Syria yaitwika lawama Israel

raia wa mji wa Damascus wamesema wamesikia milipuko wa mabomu Jumapili Desemba 7 mwaka 2014.
raia wa mji wa Damascus wamesema wamesikia milipuko wa mabomu Jumapili Desemba 7 mwaka 2014. AFP PHOTO/ANWAR AMRO

Jeshi la Syria linaishtumu Israeli kwa kutekeleza mashambulizi mawili ya angaa karibu na jiji kuu Damascus. Mashambulizi ambayo hayakusababisha hasara yoyote.

Matangazo ya kibiashara

Ripoti zimesema kuwa, ndege za kijeshi za Israeli zimetekeleza mashambulizi ya Bomu karibu na uwanja wa ndege wa kimataufa jijini Damascus na mji wa Dimas.

Jeshi la Syria katika ripoti iliyotangazwa na Televisheni ya Taifa limesema hakuna aliyeuawa wala kujeruhiwa wakati wa mashammbulizi hayo.

Si mara ya kwanza kwa Israeli kutekeleza mashambulizi kama haya nchini Syria na imekuwa ikifaya hivyo tangu mwaka 2011.

Jeshi la Syria limesema hatua hiyo ya Israeli ni kuingilia himaya ya nchi nyingine bila kibali, na kulishtumu jeshi la Israeli kuwasaidia waasi wanaoendelea kupambana na serikali ya rais Bashar Al Assad.

Shirika la kutetea haki za binadamu nchini Syria nalo limethibitisha kutoka kwa mashambulizi hayo na limesema mamshambulizi 10 yalisikiaka karibu na mji wa Dimas.

Jeshi la Israli limekataa kujibu tuhma za Syria, kwa kile linachosema huwa halizungumzi wakati linapotekeleza mashambulizi nje ya mipaka ya Israeli.