PALESTINA-ISRAEL-Usalama

Abbas ailaumu serikali ya Israel

Raia wa Palestina waandamana wakiwa na mabango yenye picha ya waziri Palestina, Ziad Abu Ein, aliyeuawa Jumatano Desemba 10 mwaka 2014.
Raia wa Palestina waandamana wakiwa na mabango yenye picha ya waziri Palestina, Ziad Abu Ein, aliyeuawa Jumatano Desemba 10 mwaka 2014. REUTERS/Ammar Awad

“ Njia zote zinawezeka”, amesema rais wa Mamlaka ya Palestina, Mahamoud Abbas kufuatia kifo cha mmoja wa viongozi wa Palestina, anayehusika na masuala ya ukoloni nchini Palestina.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa watu waliyo karibu naye, Ziad Abou Eïn, ameuawa jana Jumatano Desemba 10 katika makabiliano na jeshi la Israel wakati ambapo alikua akiandamana kwa amani.

Mjini Ramallah mamia ya raia waliandamana hadi nyumbani kwa familia ya marehemu ili kuonyesha masikitiko yao na ghadhabu waliyokua nayo.

Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas amewashtumu polisi wa Israeli kwa kumuua mmoja wa Mawaziri wake.

Waziri huyo Ziad Abu Ein, alifariki muda mfupi tu baada ya askari polisi wa Israeli aliyekuwa analinda mpaka katika eneo la Ukingo wa Magharibi kumvuta kwa nguvu huku akiwa amemshika shingo wakati wa kusambaratisha maandamano.

Kutokana na kifo hicho, shinikizo kutoka Mamlaka ya Palestina zimeanza kutolewa kwa rais Abbas kubadiisha sera yake ya kushirikiana na Israel kuhusu maswala ya usalama.

Abu Ein mwenye umri wa miaka 55, alikuwa miongoni mwa waandamanaji waliokwenda katika eneo tata la ukingo wa Magharibi kuandamana kulalamikia kile wanachosema Israel kukalia ardhi yao na kukabiliana na wana usalama wa Israeli.

Waziri wa Ulinzi wa Israeli, Moshe Yaalon, amesema anasikitika kwa kutokea kwa mauji hayo na Israel inachunguza namna mauaji hayo yalivyofanyika.

Tukio hili linakuja wakati huu kukiwa na hofu ya usalama kati ya Palestina na Israel kuhusu mji wa Jerusalem.