PALESTINA-ISRAELI-MAANDAMANO-Usalama

Hali ya wasiwasi yatanda Cisjordania

Kikosi cha ulizi wa taifa cha Plaestina kikibeba jeneza ya kiongozi Ziad Abou Eïn wakati wa mazishi yake mjini Ramallah, Desemba 11 mwaka 2014.
Kikosi cha ulizi wa taifa cha Plaestina kikibeba jeneza ya kiongozi Ziad Abou Eïn wakati wa mazishi yake mjini Ramallah, Desemba 11 mwaka 2014. REUTERS/Mohamad Torokman

Jeshi la Israel limeendelea Ijumaa Desemba 12 kuongeza idadi ya askari katika mji wa Cisjordania, siku moja baada ya mazishi ya kiongozi mmoja wa palestina mjini Ramallah.

Matangazo ya kibiashara

Ziad Abu Eïn mmoja kati ya viongozi wa chama cha Fatah na waziri wa zamani wa Palestina, aliuawa Jumatano kufuatia mshituko wa moyo wakati alipokua akiandamana kwa amani dhidi ya ukoloni wa Israel, ambao unaendelea.

Hali ya wasiwasi imeendelea kushuhudiwa katika mji wa Cisjordania.

Maandamano yamepangwa kufanyika katika mji wa Cisjordania, baada ya swala ya Ijumaa. Kwa mujibu wa kiongozi mmoja wa Fatah, chama cha Mahmoud Abbas, maandamano yamepangwa kufanyika Turmus Ayya, kijiji cha Cisjordania ambapo Ziad Abu Eïn alifariki Jumatano katika makabiliano na jeshi la Israel.

Haijafahamika iwapo maandamano hayo yataitikiwa na watu wengi au kutakuepo na kundi la watu wachache ambao wataandamana.

Kwa upande wake jeshi la Israel limeendelea kuongeza askari katika mji wa Cisjordania.

Hayo yakijiri viongozi wa Mamlaka ya Palestina wanatazamiwa kukutana ili kutathmini hatua ambazo watachukua baada ya kifo cha Ziad Abu Eïn. " Kila kitu kinawezekana", amesema Mahmoud Abbas.

Abbas ametishia kuwafungulia mashitaka viongozi wa Israel kwenye Mahakama ya kimataifa ya Jina ya ICC.

Kiongozi huyo wa Mamlaka ya Palestina amesema kuna uwezekano wa kuendelea na harakati zake kwenye taasisi za kimataifa na kuwasilisha azimio mbele ya Baraza la Usalama la Umaoja wa Mataifa la kutaka Israel isitishe kuendelea kukalia maeneo ya Palestina.