UNSC-PALESTINA-UKOLONI-HAKI

UNSC yakataa azimio la Palestina

Jumanne Desemba 30 mwaka 2014, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipiga kura dhidi ya azimio lililowasilishwa na Palestina.

Baraza la Usalama la Umoja wa MAtaifa lafutia mbali azimio lililowasilishwa na Palestina.
Baraza la Usalama la Umoja wa MAtaifa lafutia mbali azimio lililowasilishwa na Palestina. REUTERS/Eduardo Munoz
Matangazo ya kibiashara

Azimio hilo lilikua linapendekeza kusitishwa kwa mkataba wa amani na Israel ndani ya mwaka mmoja na kujiondoa kwa Israel kutoka maeneo inayoshikilia ifikapo mwaka 2017.

Marekani hawakuweka kura yao kwani nakala iliyowasilishwa na Palestina haikupata kura tisa muhimu zinazohitajika kwa ajili ya kupitishwa kwake.

Kura nane za ndio, kura mbili za hapana pamoja na mataifa matano ambayo hayakuonesha msimamo wao.

Wapalestina walijua mapema kwamba azimio hilo halitopitishwa, lakini walikua na matumaini ya angalau kupata kura tisa ili Marekani iweze kutia kura yake. Mataifa ambayo hayakuonesha msimamo wao, yamejitetea na kuisihi Palestina kutoharakia kupiga kura.

Kuharakia huko kwa Palestina kumewashangaza wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, lakini kwa upande wa mwakilishi wa Palestina, Riad Mansour, amesema kuwa msimamo wa Palestina unaeleweka.

" Wito huo wa kila mara wa sisi kusubiri wakati ambapo raia wetu wanaendelea kuteseka, wakati ambapo nchi yetu inaendelea kutawaliwa kimabavu na raia wa kigeni, wito huo hauna maana yoyote katika mazingira haya", amesema Riad Mansour.

Lakini balozi wa Marekani ameelezea msimamo wa Marekani kuwa kuanza kwa mazungumzo ya amani hayatotekelezwa kwa azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, hasa kama Palestina itaendelea kushinikiza kupitishwa kwa nguvu azimio hilo.

" Nakala hii inaeleza wasiwasi wa upande mmoja. Nakala inaunga mkono mgawanyiko na si maelewano", amesema Samanta Power.

Ufaransa ilijitahidi kuwepo na maelewano katika wiki za hivi karibuni kwa kuandaa azimio litakaloungwa mkono na Palestina pamoja na Israel.

Jumanne Desemba 30, Ufaransa imeunga mkono nakala ya Wapalestina kwa kanuni, lakini balozi wake amekumbusha kwamba Ufaransa imekua ikiendelea na jitihada zake ili kupitishwa kwa makubaliano yatakayojumuisha pande zote husika katika mwaka 2015.