JORDAN-IS-SYRIA-UGAIDI-USALAMA

IS yarusha mahojiano ya rubani wa Jordan

jawat Kasasbeh, ndugu wa rubani wa Jordan anayeshikiliwa na kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam, akiwa katika Sala, mjini Amman.
jawat Kasasbeh, ndugu wa rubani wa Jordan anayeshikiliwa na kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam, akiwa katika Sala, mjini Amman. REUTERS/Muhammad Hamed

Kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam limerusha hewani mahojiano iliyofanya na rubani wa Jordan anaeshikiliwa na kundi hilo tangu juma lililopita nchini Syria wakati ndege yake ilipoanguka katika mji wa Raqqa, nchini Syria.

Matangazo ya kibiashara

Mahojiano hayo yamechapishwa katika mtandao wa jarida la El Dabiq. Rubani huyo ambaye bado kijana, ameelezea kwa nini aliweza kuendesha mashambulizi dhidi ya ngome za kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam.

Ndege aliyokua akiendesha rubani huyo ilishambuliwa kwa kombora liliyorushwa na kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam, taarifa ambayo inaendana na ile iliyotolewa na wanajihadi kwamba wao ndio walioishambulia kwa kombora ndege hio ya Jordan.

Rubani huyo anachukuliwa na kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam kama rubani potofu kwa sababu amekua akishiriki katika vita vinavyoendeshwa na muungano wa kimataifa unoongozwa na Marekani dhidi ngome zao.

Moath Kasasbeh amethibitisha kuwa ndege yake F-16 ilishambuliwa kwa kombora. Taarifa ambayo ilikanushwa na uongozi wa Marekani katika muungano wa kimataifa dhidi ya Kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam.

Mahojiano haya yamechapishwa wakati kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam limetoa masharti ya kuachiliwa kwa rubani huyo.

Kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam limeitaka Jordan kuondoka na kuwaondoa wanajeshi wake katika muungano wa kimataifa pamoja na kuachiliwa huru kwa wafungwa kadhaa.

" Nina imani kwa serikali ya Jordan, amesema Jawat Kasasbeh", ndugu wa rubani anayeshikiliwa na kundi la wapiganaji wa Doala la Kiislam.

" Ndugu yangu alifuata tu amri ya jeshi. Kwa hivyo basi, ni serikali kufanya kinachowezekana ili kumuokoa ndugu yangu. Ingawa masharti ni mazito upande wa serikali, nina imani kuwa serikali itafanya kinachowezekana ili Moath arejeye nchini. Niina uhakika kuwa Jordan itaondoka muungano", ameongeza Jawat Kasasbeh.