PALESTINA-ICC-ISRAEL-HAKI ZA BINADAMU-SHERIA

Palestina yaiomba ICC kuchunguza uhalifu uliyotokea Gaza

Wazir9i mkuu wa Israel Benyamin Netanyahu (kushoto), akiwa pamoja na rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas (kulia), mwaka 2010 katika mji wa Jérusalem.
Wazir9i mkuu wa Israel Benyamin Netanyahu (kushoto), akiwa pamoja na rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas (kulia), mwaka 2010 katika mji wa Jérusalem. AFP PHOTO/ALEX BRANDON-POOL

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita ICC, yenye mako yake mjini Hague, Uholanzi, imeiponzgeza Palestina kwa uamzi iliyochukua.

Matangazo ya kibiashara

Mahakama hiyo ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita ICC,imesema Mamlaka ya Palestina imetambua uwezo wake wa kuchunguza kuhusu uwezekano wa kutokea kwa visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu katika eneo la Gaza mwaka uliopita.

ICC imesema inatambua kuwa ina jukumu la kuchunguza ikiwa wanajeshi wa Isreal walitekeleza uhalifu wakati wa Operesheni yao katika eneo hilo lakini Mahakama hiyo imeweka wazi kuwa kutambua huko hakumaanishi kuwa itaanza mara moja uchunguzi huo.

Palestina iliomba kuwa mwanachama wa Mahakama hiyo, ombi ambalo bado linatathminiwa na Umoja wa Mataifa.

Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu amesema hatakubali wanajeshi wake kushatakiwa katika Mahakama hiyo ikiwa Palestina itakubaliwa kuwa mwanachama.