Pata taarifa kuu
ISRAEL-SYRIA-HEZBOLLAH-MAUAJI-MAPIGANO-USALAM

Maafisa wa Hezbollah wauawa katika milima ya Golan

Askari wa Israel wakiwa katika milima ya Golan, wanaelekeza macho yao nchini Syria.
Askari wa Israel wakiwa katika milima ya Golan, wanaelekeza macho yao nchini Syria. REUTERS/Ronen Zvulun
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Jeshi la Israel limeendesha mashambulizi Januari 18 katika milima ya Golan nchini Syria. Wapiganaji wa Hezbollah kutoka Libanon wameuawa katika mashambulizi hayo.

Matangazo ya kibiashara

Hii si mara ya kwanza tangu yalipoanza machafuko nchini Syria miaka minne iliyopita, jeshi la Israel kushambulia maeneo muhimu ya Syria.

Mashambulizi ya Jumapili Januari 18 yalifanyika karibu na kijiji cha Mazraat al-Amal, katika jimbo la Quneitra, linalopakana na milima wa Golan nchini Syria, ambayo inakaliwa na Israel.

Helikopta za jeshi la Israel zikiongozwa na magari ya kijeshi zilirusha makombora mawili, anasema Paul Khalifeh, mwandishi wa RFI katika mji wa Beirut. Wakati huo huo, ndege mbili zisiyo na rubani zimekua zikiruka juu ya eneo hilo.

Hezbollah kutoka Libanon imefahamisha mapema kwamba wapiganaji wake sita waliuawa katika mashambulizi hayo ya Israel, ikiwa ni pamoja na Mohammed Issa, mmoja kati ya maafisa wakuu wa Hezbollah nchini Syria. Jihad Mughnyeh, mwanae Imad Mughnyeh, kiongozi wa kijeshi wa Hezbollah aliye uawa katika shambulio ililiodaiwa kutekelezwa na Israel katika mji wa Damascus mwaka 2008, ni miongoni pia mwa waliouawa.

Haijafahamika iwapo Hezbollah itajilipiza kisase. Hata hivyo, kiongozi wa kundi la Hezbollah, Hassan Nasrallah, aliwahi kutoa vitisho dhidi ya serikali ya kiyahudi kwamba watajilipiza kisase kama jeshi la Israel litaendesha mashambulizi mapya katika ardhi ya Syria.

Nassrallah alisema kwamba kundi lake lina makombora ambayo yanaweza kurushwa hadi nchini Israel.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.