Pata taarifa kuu
LEBANON-ISRAELI-MASHAMBULIZI-USALAMA

Israeli na Lebanon, hofu ya mapigano mapya

Magari ya yakiteketea kwa moto karibu na kijiji cha Ghajarkwenye mpaka wa Israel na Lebanon, Januari 28 mwaka  2015.
Magari ya yakiteketea kwa moto karibu na kijiji cha Ghajarkwenye mpaka wa Israel na Lebanon, Januari 28 mwaka 2015. REUTERS/Maruf Khatib
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 2

Katika ngome kuu za Hezbollah katika mji wa Beirut na kusini mwa Lebanon, raia wamekaribisha mashambulizi dhidi ya wanajeshi wa Israeli waliokua wakipiga doria.

Matangazo ya kibiashara

Lakini kwengineko nchini Lebanon, ni hofu tu ambayo imeendelea kutanda. raia wa Lebanon wana hofu ya kutokea kwa machafuko makubwa wakati jeshi la Israeli litakusudia kulipiza kisase.

Hali hiyo inaweza kusababisha vita katika nchi hizo mbili, kama mwaka 2006. Mawanajeshi mmoja wa vikosi vya Umoja wa Mataifa nchini Lebanon Unifil ameuawa. Kwenye mpaka wa Lebanon, raia wa Israel pia wana wasiwasi ya kuzuka kwa machafuko.

Kwa mujibu wa mwandishi wa RFI katika mji wa Beyrouth, Paul Khalifeh na mwanahabari wetu aliyetumwa kwenye mpaka wa Israeli na Lebanon, Murielle Paradon, fataki zimekua zikipigwa, huku kukionekana misafara ya magari ... Lebanon, wafuasi wa Hezbollah wamesheherekea kile walichokiona kama ulipizaji kisase kwa mashambulizi ya angani ya Israeli yaliyowaua wanachama sita wa kundi hilo mnamo Januari 18 mwaka 2015 karibu na Golan.

Jamii ya wanasiasa nchini Lebanon, wametoa hisia tofauti kuhusiana na shambulio hilo la Hezbollah dhidi ya wanajeshi wa Israeli.

Waziri mkuu Tammam Salam ameonyesha wasiwasi wake kuhusu nia ya uchokozi wa viongozi wa Israel ambao walihusika, kwa mujibu wa kiongozi huyo, na kuongezeka kwa machafuko kati ya nchi hizi mbili ambayo yamefuatiwa na shambulio hilo la Hezbollah .

Waziri mkuu huyo wa Lebanon alikuwa akimaanisha mabomu yaliyorushwa na jeshi la Israel dhidi ya mikoa ya Lebanon.

Kiongozi wa jamii ya Wadruze, Walid Jumblatt alikuwa na wasiwasi ya awamu ya mabadiliko makubwa. Kiongozi huyo alimkosoa Benjamin Netanyahu, Waziri mkuu wa Israeli, ambaye alisababisha matukio hayo kwa kushambulia Hezbollah karibu na eneo la Golan kwa ajili ya mambo ya uchaguzi.

Lakini kiongozi wa kikristo, Samir Geagea si haungi mkono maoni hayo. Greagea ameelezea masikitiko yake kwamba jeshi na raia wa Lebanon wanaweza kupata madhara makubwa kufuatia uamzi huo uliyochukuliwa na Hezbollah peke yake.

Chama kikuu cha Kisuni, ambacho kimekua kikiikosoa Hezbollah, kimejizuia kueleza chochote. chama hicho kimekumbuka kuwa uamuzi wa amani na vita ni wajibu wa serikali.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.