Jordan imewanyonga wanamgambo wa IS
Imechapishwa: Imehaririwa:
Serikali ya Jordan imesema imewaua kwa kuwanyonga wanajihadi wawili raia wa Iraq ambao ni washirika wa karibu wa kundi la Kiislamu la Islamic State.
Watu hao wamekua wakizuiliwa jela nchini Jordan, kwa tuhuma za kushirikiana na kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu
Hatua hii imechukuliwa baada ya kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu kumuua kwa kumchoma moto rubani wa Jordan Maaz al-Kassasbeh waliyekuwa wanamshikilia.
Msemaji wa serikali ya Jordan amethibitisha kunyongwa kwa wawili hao ambao ni mlipuaji wa kujitoa mhaga Bi Sajida al-Rishawi na Ziad al-Karboli.
Kitendo cha kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu kuumua kwa kumchoma moto rubani wa Jordan kimelaaniwa Kimataifa, na kumlazimu Mfalme Abdullah aliyekuwa ziarani nchini Marekani kusitisha ziara hiyo.
Rais Barack Obama ni miongoni mwa viongozi wa dunia waliolaani mauji hayo.