JORDAN-IS-UGAIDI-USALAMA

Jordan yatekeleza mashambulizi dhidi ya IS

Ndege za kivita ziliyoendesha mashambulizi dhidi ya ngome za kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu. ce jeudi pour les premières représailles militaires contre le groupe EI à Raqqa en Syrie.
Ndege za kivita ziliyoendesha mashambulizi dhidi ya ngome za kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu. ce jeudi pour les premières représailles militaires contre le groupe EI à Raqqa en Syrie. REUTERS/Petra News Agency

Serikali ya Jordan imetangaza kufanya mashambulizi ya anga dhidi ya ngome za kundi la wapiganaji wa kiislamu wa Islamic State baada ya kuahidi kulipiza kisasi baada ya mauaji ya rubani wake wa kijeshi juma hili.

Matangazo ya kibiashara

Duru za Kijeshi za Jordan zinasema kuwa ndege kadhaa za kivita zililenga kambi za Islamic State hapo jana hasa ile ya mafunzo ya vikundi hivyo vya kigaidi pamoja na ghala za silaha na kusema kuwa baada ya maangamizi hayo ndege zao zimerudi salama nyumbani.

Aidha, katika mashambulizi hayo, nchi ya Marekani imetoa msaada wa kijeshi wa ndege aina ya F-16 na F-22 kwa ajili ya usalama wa ndege za Jordan pamoja na msaada wa mafuta wamesema maofisa wa Marekani.

Leo Ijumaa, maandamano yanatarajiwa kufanyika nchi nzima kuonyesha mshikamano na familia ya rubani aliyeuawa kwa kuchomwa moto na ambapo mfalme wa Jordan Abdullah II akiambatana na Waziri mkuu Abdullah Nsour, alitembelea siku ya Alhamisi familia ya rubani huyo kwenye umbali wa kilomita 120 kutoka Amman, ambapo hema kubwa imejengwa kupokea rambirambi.

Tayari nchi ya Jordan imewaonya wanajihadi wawili wa Iraq waliokuwa wamepanga mashambulizi ya kigaidi katika nchi yao.