SYRIA-NUSRA RFONT-MAPIGANO-USALAMA

Kamanda wa Nusra Front auawa Syria

Maafisa wa jeshi la serikali nchini Syria wamesema jeshi limemuua kamanda wa kijeshi kutoka kundi la waasi lenye uhusiano na Al Qaeda, la Nusra Front.

Wafuasi wa  Nusra Front, katika mji wa Deir Ezzor,Februari 25 mwaka 2013.
Wafuasi wa Nusra Front, katika mji wa Deir Ezzor,Februari 25 mwaka 2013. AFP PHOTO/ZAC BAILLIE
Matangazo ya kibiashara

Imearifiwa kuwa Watu wasiopungua 18 wameuawa mjini Aleppo, huko Syria, baada ya bomu kurushwa kutoka kwenye helikopta ya serikali.

Kwa mujibu wa shirika la kuchunguza haki za binadamu Syria lenye makao yake makuu London, waasi walikuwa wamechimba njia chini ya jengo hilo na kisha wakalipua bomu ambalo lilisababisha sehemu ya jengo kubomoka.

Nusra front ni moja kati ya makundi yenye nguvu yanayopambana ili kumuuuangusha utawala wa Bashar Al Assad, kundi hilo pia lilihusika na shambulio katika mji wa Aleppo siku ya jumatano.

Hayo yakiarifiwa mapigano makali yameendelea katika mji wa Allepo nchini Syria kati ya wanajeshi wa serikali na waasi.

Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani John Kerry amesema shinikizo za kijeshi zinahitajika ili kumwondoa madarakani rais Bashar al Assad, wito unaokuja wakati huu Urusi ikijiandaa kuongoza mazungumzo ya amani kati ya serikali na wasi mwezi ujao.

Upinzani kwa upande wake umesema sio lazima kuondolewa kwa rais Assad kabla ya mazungumzo ya amani kuanza.