PALESTINA-ISRAELI-PLO-USHIRIKIANO-USALAMA

PLO yasitisha ushirikiano wake wa kiusalama na Israel

Katibu mkuu wa PLO, Yasser Abed Rabbo, Ramallah, Oktoba 16 mwaka 2014.
Katibu mkuu wa PLO, Yasser Abed Rabbo, Ramallah, Oktoba 16 mwaka 2014. AFP PHOTO/ABBAS MOMANI

Taasisi muhimu ya chama cha PLO imeamua Alhamisi usiku Machi 5 kuvunja ushirikiano wa kiusalama na Israeli. Uamuzi huu hautatekelezwa wakati huu lakini unaweza kuwa na madhara makubwa.

Matangazo ya kibiashara

Kusitishwa kwa ushirikiano wa kiusalama kati ya Wapalestina na Waisraeli kunaweza kusababisha mvutano mkubwa katika nchi hizi mbili. Kama kwa mfano vikosi vya Palestina vikiondoka katika maeneo yalio chini ya udhibiti wao katika ukingo wa Cisjordania, na kuwaachia nafasi Waisareli. Chanzo kingine cha wasiwasi kwa Israeli : kama Idara ya ujasusi ya Palestina ikisitisha kuendelea kupeana taarifa na Israeli, hususan taarifa muhimu ya kiupelelezi kwa kuzuia mashambulizi hayo, huenda hali ikawa mbaya zaidi katika ukingo huo wa Cisjordania..

Kwa mujibu wa waandishi wa RFI, katika mji wa Ramallah, Murielle Paradon na Nicolas Ropert, Palestina imekua ikitishia mara kadhaa kusitisha ushirikiano wake wa kiusalama na Israeli, bila hata hivyo kutekeleza jambo hilo. PLO imeeleza kwamba imekua ikishuhudiwa mashambulizi ya angani ambayo yamekua yakitekelezwa mara kwa mara na jeshi la Israeli katika ukingo wa Cisjordania, huku Palestina ikiendelea kuathirika kutokana na uamzi wa Israeli wa kuzuia malipo ya ushuru.

“ Israeli tunaidai zaidi ya Euro milioni 400 ya malipo ya ushuru. Na imejizuia kulipa pesa hiyo. Je tuna kesi na taifa la Israeli au tuna kesi na kundi la wahuni?, amejilaumu kiongozi wa Mamlaka ya Palestina, Mahmoud Abbas, Alhamisi katika mkutano wa kamati kuu ya PLO.