ISAELI-UCHAGUZI-SIASA

Siku ya uchaguzi Israeli: mrengo wa kati-kushoto waongoza

Yitzhak Herzog (kushoto) na Tzipi Livni (kulia), wote hao ni viongozi wa chama cha mrengo wa kati-kushoto, wakijaribu kuwashawishi wapiga kura, kwenye makao yao makuu katika mji wa Tel Aviv, Machi 15 mwaka 2015.
Yitzhak Herzog (kushoto) na Tzipi Livni (kulia), wote hao ni viongozi wa chama cha mrengo wa kati-kushoto, wakijaribu kuwashawishi wapiga kura, kwenye makao yao makuu katika mji wa Tel Aviv, Machi 15 mwaka 2015. REUTERS/Nir Elias

Wananchi wa Israeli Jumanne asubuhi wiki hii wanaanza kupiga kura kuwachagua wabunge, na chama kitachoshinda kitaunda serikali.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa mwandishi wa RFI, Jerusalem, Nicolas Falez, ushindani ni kati ya chama cha Waziri Mkuu wa sasa Benjamin Netanyahu wa chama cha Likud na Isaac Herzog wa chama cha mrengo wa kati-kushoto cha Kiyazuni.

Kuelekea uchaguzi wa leo, kura za maoni zimekuwa zikimpa nafasi kubwa kiongozi wa upinzani bwana Herzog lakini wadadisi wa mambo wanasema huenda chama cha Netanyahu kikawa na ushawishi wa kuomba muungano wa vyama vingine baada ya uchaguzi wa leo.

Hata hivyo Waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu ameapa kuwa hakutakua na taifa huru la Palestina kama atakua bado madarakani.

Kakini msimamo wa chama cha mrengo wa kati-kushoto cha Isaac Herzog, kimebaini kwamba kuundwa kwa taifa huru la Palestina kutapelekea Israeli inakua taifa la Kiyahudi na lenye misingi ya kidemokrasia.