SYRIA-MASHAMBULZI

Human Rights Watch yawatuhumu waasi na serikali ya Syria kutekeleza mauaji kimakosa

Shirika la kimataifa linalo tetea haki za binadamu la Human Right Watch limesema, wapiganaji wanaoipinga serikali ya Syria pamoja na wanajihadi wanaoungwa mkono na maitaifa ya magharibi wameshambulia kimakosa raia wa kawaida, ikiwani uvunjifu wa haki za binadamu.

wananchi wa jiji la Damascus wakisubiri misaada ya kibinadamu
wananchi wa jiji la Damascus wakisubiri misaada ya kibinadamu REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Katika ripoti iliochapishwa hii leo na shirika hilo lenye makao yake makuu jijini New York, limechambua kwa kina matukio kadhaa ya mashambulizi ya waasi wa Syria dhidi ya maeneo yanayo milikiwa na serikali ya rais Bashar Al Assad.

Naibu mkurugenzi wa Human Right Watch katika ukanda wa mashariki ya kati Nadim Houzy amesema wanaendelea kushuhudia mbio za waasi kwenye safa ya mwanzo pamoja na ukatili wa majeshi ya serikali dhidi ya raia wa kawaida katika maeneo yanayodhibitiwa na waasi na yale yaliopo chini ya himaya ya serikali, huku jumui ya kimataifa ikikaa kimya.

Human Right Watch imefanya uchunguzi pia kuhusu mashambulizi ya kujitowa muhanga yaliotokea katika mji wa Damascus pamoja na Homs yaliolenga vituo vya jeshi ambapo asilimia kubwa ya mashambulizi hayo ni kuzidisha hodu miongoni mwa raia wa kawaida, moja miogoni mwa matukio hayo lilitokea Octoba mwaka jana nje ya shule moja katikati mwa jiji la Homs na kuwauwa watoto 45.

kulingana na ripoti hiyo ya Human right Watch, miongoni mwa makundi yanayohusika na na shambulio hilo la kimakosa ni kundi la islamic State pamoja na waasi wa jeshi huru la Syria linaloungwa mkono na mataifa ya magharibi.

Takriban mashambulizi 10 yalithibitishwa kutekelzwa na Islamic State au kundi la Al Nosra, kitengo cha Alqeda nchini Syria, lakini pia waasi wa jeshi huru la Syria walikiri kuhusika na mashambulizi ya milipuko katika maeneo ya raia wa kawaida jijini Damsacus imesema ripoti hiyo ya Human Right Watch.

Human Right watch imesema makundi ya upinzani yanasema kwamba ni halali kwao kufanya mashambulizi katika maeneo yanayomilikiwa na serikali, lakini hii sio halali upande wa haki za binadamu, hivyo shirika hilo limetowa wito kwa pande zote kusitisha mashambulizi dhidi ya raia wasiokuw ana hatia yoyote.

Watu zaidi ya 215.000 wanakadiriwa kupoteza maisha nchini Syria tangu kuanza kwa machafuko nchini humo March mwaka 2011 yalioanza kwa maandamao kabla ya kuingia katika mapigano ya wenyewe kwa wenyewe. Serikali ya Syria nayo pia inatuhumiwa kwa makosa ya mashambulizi dhidi ya maeneo ya raia wasiokuw ana hatia yoyote lakini pia vitendo vya unyanyasaji na matumizi ya bomu za sumu.