ISRAELI-SIASA

Netanyahu aomba msamaha Waarabu wenye asili ya Kiisraeli

Waziri mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu, Tel Aviv, MAchi 18 mwaka 2015, akiwa na mke wake.
Waziri mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu, Tel Aviv, MAchi 18 mwaka 2015, akiwa na mke wake. REUTERS/Nir Elias

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amepata uungwaji mkono mkubwa kuunda serikali ya mseto.

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa ofisi ya rais ameliambia shirika la habari la AFP kwamba rais Reuven Rivlin anakamilisha mazungumzo ya siku mbili pamoja na wawakilishi wa vyama 10 vilivyoko bungeni kusikiliza nani wanaempendekeza kuwa waziri mkuu, ambapo vyama sita vimemuunga mkono Netanyahu.

Msemaji wa rais Jason Pearlman ameliambia shirika la habari la AFP kwamba rais amekutana hivi karibuni na chama cha Yisrael Beitenu na wamempendekeza Netanyahu na kufikisha jumla ya wabunge 67 miongoni mwa bunge lenye wabunge 120 ambao wanamuunga mkono kiongozi huyo wa Israel.

Duru za kuaminika zinabaini kwamba Benjamin Netanyahu anatazamiwa kuteuliwa wiki hii kuwa waziri mkuu wa Israeli, baada ya kuungwa mkono na wabunge wengi.

Hata hivyo, Netanyahu ameomba msamaha jamii ya waarabu wenye asili ya Kiisraeli. Juam lililopita, alilaani “tishio kufuatia uhamasishaji wao katika uchaguzi wa Machi 17.