Syria : HRW yanyooshea kidole cha lawama serikali na waasi
Imechapishwa:
Watu wasiopungua kumi na wawili wameuawa na wengine takribani thelathini wamejeruhiwa katika shambulizi lililotekelezwa na waasi katika mji wa pili kwa ukubwa wake nchini Syria wa Aleppo.Televisheni ya taifa imeripoti.
Hayo yanajiri wakati Shirika la kimataifa linalotetea haki za binadamu, Human Right Watch limesema, wapiganaji wanaoipinga serikali ya Syria pamoja na wanajihadi wanaoungwa mkono na maitaifa ya magharibi wameshambulia kimakosa raia wa kawaida, ikiwa ni uvunjifu wa haki za binadamu.
Katika ripoti iliochapishwa mwanzoni mwa juma hili shirika hilo lenye makao yake makuu jijini New York, limechambua matukio kadhaa ya mashambulizi ya waasi wa Syria dhidi ya maeneo yanayo milikiwa na serikali ya rais Bashar Al Assad.
Hayo yakijiri kundi la wapiganaji wa Dola la kiislamu limeendesha mashambulizi ndani ya masaa 24 yaliyopita na kuwaua wapiganaji kadhaa wa Kikurdi. Wanamgambo wa kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu wameendesha mashambumbilizi katika maeneo tofauti dhidi ya jeshi la Syria hususan katika mikoa ya Hama na Homs, katikati mwa nchi ya Syria.