SAUDI ARABIA-YEMEN-VITA--SIASA

Saudi Arabia yaanzisha operesheni ya kijeshi Yemen

Les bombardements de l'opération «Tempête de fermeté» sur Sanaa, la capitale du Yémen, ont fait des victimes ce jeudi 26 mars.
Les bombardements de l'opération «Tempête de fermeté» sur Sanaa, la capitale du Yémen, ont fait des victimes ce jeudi 26 mars. REUTERS/Khaled Abdulla

Saudi Arabia imeanzisha operesheni ya kijeshi katika nchi ya Yemen, wakati ambapo mji mkuu wa nchi hiyo ukiendelea kushikiliwa na waasi wa Kishia kutoka jamii ya Houthi, ametangaza balozi wa Saudi Arabia nchini Marekani.

Matangazo ya kibiashara

Mataifa kumi yanaunga mkono operesheni hiyo, ambayo inajulikana kwa jina la “ Dhoruba iliyo imara”. Mbali na nchi tano za Ghuba na Misri ambazo zimethibitisha rasmi kushiriki katika operesheni hiyo, Marekani, Morocco, Jordan, Pakistan na Sudan pia zinasadikiwa kushiriki katika operesheni hiyo ambayo imeanzishwa na Saudi Arabia.

Mashambulizi hayo ya Saudi Arabia katika aridhi ya Yemen yanasadikiwa kuwa yemeshawaua watu kumi na tatu kwa mujibu wa mamlaka ya ulinzi ya Yemen ambayo imenukuliwa mapema Alhamisi asubuhi wiki hii na shirika la habari la Ufaransa AFP.
Moja ya maeneo ya mji wa Sanaa limeshambuliwa kwa mabomu. Inaarifiwa kuwa huenda kuna miili ya watu ambayo bado iko chini ya vifusi, kwa mujibu wa mashahidi.

“ Operesheni hii inalengo la kutoa ulinzi kwa serikali halali ya rais wa Yemen Abd Rabbo Mansour Hadi”, balozi wa Saudi Arabia nchini Marekani, Adel al-Jubeir, ametangaza katika mkutano na vyombo vya habari.

Operesheni hii itajikita kwa mashambulizi ya angani peke, lakini vikosi vingine vya kijeshi vimewekwa tayari. Kwa mujibu wa balozi Adel al-Jubeir, muungano unaoundwa na mataifa kumi utafanya kilio chini ya uwezo wao ili kurejesha madarakani serikali halali.

Ndege za kivita F15 za Saudi Arabia katika mazoezi kwenye anga ya Riyad, mjimkuu wa Saudi Arabia.
Ndege za kivita F15 za Saudi Arabia katika mazoezi kwenye anga ya Riyad, mjimkuu wa Saudi Arabia. AFP PHOTO/HASSAN AMMAR

Operesheni hii ilianza saa tano usiku Jumatano wiki hii. Kwa mujibu wa baadhi ya vyanzo, ndege za kivita zimeendesha mapema usiku wa Jumatano shambulio dhidi ya uwanja wa ndege wa Sanaa. Mashahidi na vyanzo vya kijeshi vimebaini kwamba mashambulizi ya Saudi Arabia yamelenga maeneo muhimu yanayoshikiliwa na waasi wa Kishia katika mji wa Sanaa, ikiwemo kambi kuu ya waasi hao katika mji wa Al-Daïlami, kaskazini mwa mji mkuu, pamoja na kambi nyingine ya vikosi maalumu. Kwa mujibu wa vyanzo hivyo moto ulizuka katika ikulu ya rais.

Kwa mujibu wa televisheni Al Arabiya iliyonukuliwa na Reuters, ndege 100 za kijeshi za Saudi Arabia pamoja na wanajeshi 150,000 wanashiriki katika operesheni hii. Ndege za kivita za Misri, Morocco, Jordan, Sudan, Koweit, Umoja wa falme ya Kiarabu, Qatar na Bahreïn zinashiriki katika operesheni hii, kwa mujibu wa televisheni ya Al Arabiya.