YEMEN-SAUDI ARABIA-VITA-SIASA

Yemen : wapiganaji wa Houthi waingia Aden

Wapiganaji wa Kishia kutoka jamii ya Houthi katika mji wa Sanaa, Machi 28 mwaka 2015.
Wapiganaji wa Kishia kutoka jamii ya Houthi katika mji wa Sanaa, Machi 28 mwaka 2015. REUTERS/Khaled Abdullah

Wapiganaji wa kundi la waasi wa Kishia kutoka jamii ya Houthi waliingia Jumatano wiki hii katikati mwa mji wa Aden, mji wa pili mkubwa nchini Yemen.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa mashahidi, waasi wa Kishia wamefaulu kuingia katikati mwa mji huo mkuu wenye bandari kusini mwa Yemen kwa usaidizi wa kikosi cha wanajeshi wa jeshi la Yemen ambao wameendelea kumtii rais wa zamani Ali Abdallah Saleh.

Kwa mujibu wa mwandishi wa RFI, mjini Riadh, Clarence Rodriguez, kwa muda wa juma moja mashambulizi ya anga yanayoendeshwa na Saudi Arabia yameendela kulenga ngome kuu za Houthi, hususan maeneo muhimu, makambi ya jeshi ambako kunahifadhiwa silaha na makombora mengine.

Kaskazini na Kusini mwa Yemen, waasi wa Kishia kutoka jamii ya Houthi wanaendelea kushiikilia baadhi ya maeneo. Waasi hao wameendelea kuhimili mashambulizi ya muungano unaoongozwa na Saudi Arabia. Mashambulizi hayo yamesababisha vifo vya watu wengi, mkiwemo raia wa kawaida.

Waasi hao wa Kishia waliingia katika mji wa Aden wakiwa na magari yao ya kijeshi pamoja na vifaru. Wameteka majengo ya serikali katika eneo la Khor Maksar, linalounganisha mji wa Aden na maeneo mengine.

Waasi wa Kishia wakishirikiana na baadhi ya wanajeshi wa jeshi la Yemen ambao bado wanamtii rais wa zamani Ali Abdallah Saleh, wameendelea kuyateka baadhi ya maeneo, licha ya mashambulizi makali ya muungano unaoongozwa na Saudi Arabia.

Mji wa Aden umeendelea kulengwa na mashambulizi ya waasi tangu rais Abd Rabbo Hadi Mansour alipoondoka katika mji huo na kukimbilia Saudi Arabia.

Waziri wa mambo ya nje wa Yemen, Ryad Yassine, ambaye alikimbilia pia Saudi Arabia ameomba akisisitiza muungano unaoendesha vita dhidi ya waasi wa Kishia kuamuru majeshi yao kuanzisha vita vya aridhini, akibani kwamba mashambulizi ya angani hayatozaa matunda yoyote.