SYRIA-IS-USALAMA

Syria : Wakurdi 300 watekwa nyara na wanajihadi

Takriban Wakurdi 300, ambao walikua wakijielekeza katika mji wa Aleppo kaskazini mwa Syria, kupata malipo yao ya mishahara, wametekwa nyara na waasi wa kiislamu, Jumatatu wiki hii, Magharibi mwa mji huo,vyanzo Kikurdi vimesema.

Wanamgambo wa kiislamu wawateka nyara Wakurdi 300 katika kijiji cha Kikurdi cha Afrin.
Wanamgambo wa kiislamu wawateka nyara Wakurdi 300 katika kijiji cha Kikurdi cha Afrin. Reuters
Matangazo ya kibiashara

" Kundi la watu 300 waliokua ndani ya mabasi matano na basi ndogo la abiria wakitokea katika kijiji cha Kikurdi cha Afrin wametekwa katika eneo la waasi wa kiislamu, wakati ambapo walikua wakielekea Aleppo kupokea mishahara yao," Nawaf Khalil, msemaji wa chama cha PYD barani Ulaya, ameliambia shirika la hbari la Ufaransa AFP.