YEMEN-SAUDI ARABIA-HOUTHI-VITA-SIASA

Zaidi ya watu 110 wauawa kusini mwa Yemen

Mapigano yanayoendelea kushuhudiwa Yemen yameendelea kusababisha vifo katika maeneo mbalimbalimbali ya nchi hio.
Mapigano yanayoendelea kushuhudiwa Yemen yameendelea kusababisha vifo katika maeneo mbalimbalimbali ya nchi hio. REUTERS/Nabeel Quaiti TPX IMAGES OF THE DAY

Mapigano mapya yameibuka kusini mwa Yemen kati ya waasi wa Kishia kutoka jamii ya Houthi na wafuasi wa rais anayeungwa mkono na Saudi Arabia.

Matangazo ya kibiashara

Mapigano hayo yamesababisha vifo vya watu 110, wakati ambapo shirika la msalama mwekundu linakabiliwa na tatizo la kusafirisha msaada wa kiutu.

Kwa siku ya kumi na mbili ya operesheni ya muungano unaoongozwa na Saudi Arabia dhidi ya waasi wa Kishia, mapigano makali yamekua yakiendelea kusini mwa Yemen, ambapo watu 114 wanaarifa kuuawa, ikiwa ni pamoja na 53 katika mji wa Aden, mji wa pili wa nchi hio, kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali nchini Yemen.

Hata hivyo hali ya kibinadamu imeendelea kuwa tete sasa baada ya saa, wakati ambapo hospitali nchini humo zinakabiliwa na uhaba wa dawa, huku mamia ya watu wakiwa wamejeruhiwa.

Mpaka sasa hakuna msaada kutoka mataifa ya kigeni. Shirika la msalaba mwekundu limebaini Juamtatu wiki hii kwamba linakabiliwa na uwezo wakusafirisha madawa na vifaa mbalimbali.

“ Tumeruhusiwa kusafirisha vifaa mbalimbali vya hospitali ambavyo vimo katika ndege ya mizigo, lakini bado kuna tatizo kuhusu wapi ndege hiyo itatua, kwani katika mji wa Sanaa ambapo ndege hio ingelitua, bado kuna mapigano”, amesema msemaji wa shirika la msalaba mwekundu, Sitara jabeen.

Kwa mujibu wa shirika la msalaba mwekundu, karibu tani 48 za dawa na vifaa mbalimbali vya upasuaji vinasubiri kusafirishwa kwa ndege au kwa meli.

Hali ya Usalama imeendelea kudorora katika mji wa Aden. Mapigano ya Jumapili mwishoni mwa juma hili yaligharimu maisha ya watu wa kawaida 17 na wapiganaji 10 wanaomtii rais Abd Rabbo Mansour Hadi aliyekimbilia Riad, chanzo cha hospitali kimebainisha.

Kwa upande wake, chanzo cha kijeshi kimetoa idadi ya waasi 26 wa Houthi wanoungwa mkono na Iran, ambao waliuawa.