SYRIA-MAZUNGUMZO-USALAMA-SIASA

Mazungumzo ya kusaka amani Syria yanaendelea

Rais wa Syria Bashar Al-Assad.Mazungumzo kati ya utawala wa Bashar Al-Assad na waasi yanaendelea Moscow, Urusi.
Rais wa Syria Bashar Al-Assad.Mazungumzo kati ya utawala wa Bashar Al-Assad na waasi yanaendelea Moscow, Urusi. Reuters/Sana/Handout

Mazungumzo yenye lengo la kumaliza vita nchini Syria yaliyoanza Jumatatu wiki hii mjini Moscow, nchini Urusi yanaingia katika siku yake ya pili leo Bila ya kuwepo kwa makundi muhimu ya upinzani.

Matangazo ya kibiashara

Balozi wa Syria katika Umoja wa Mataifa, Bashar Al-Jaafari anayeongoza ujumbe wa serikali katika mkutano huo amesema anahisi kutakuwa na matumani finyu ya kutatua mgogoro wa taifa hilo.

Lakini kundi kubwa la muungano wa upinzani lenye kuungwa mkono na mataifa ya Magharibi la nje ya Syria limejiweka kando, wakati kundi jengine lenye kuongoza harakati za upinzani bado limo katika marufuku ya kusafiri nje ya Syria iliyowekwa na serikali ya taifa hilo .

Mazungumzo haya ambayo yataendelea mpaka April 9, yanatarajiwa kujikita zaidi katika masuala ya kiutu na mipango ya mazungumzo ya siku za usoni, ambayo vilevile yanaonekana kama yanafungua njia kwa Urusi, taifa lenye kuunga mkono serikali ya Syria, kujenga taswira yake kama mpatanishi muhimu wa mgogoro wa Syria.