UNSC-YEMEN-SAUDI ARABIA-HOUTHI-VITA-SIASA

UNSC yatazamia kupitisha vikwazo dhidi ya waasi wa Huthi

Mwanajeshi wa Saudi Arabia katika mji wa Jizan, katika mpaka kati ya Yemen na Saudi Arabia, Aprili 13 mwaka 2015.
Mwanajeshi wa Saudi Arabia katika mji wa Jizan, katika mpaka kati ya Yemen na Saudi Arabia, Aprili 13 mwaka 2015. RFI / Clarence Rodriguez

Baraza la Usalama za Umoja wa Mataifa linakutana leo Jumanne kupitisha azimio kuhusu mapigano yanayoendelea nchini Yemen.

Matangazo ya kibiashara

Azimio hilo linalenga kuwawekea vikwazo vya silaha waasi wa Kishia lakini pia kuwawekea vikwazo viongozi wa kundi hilo na washirika wao.

Hata hivyo kuna wasiwasi kuwa huenda azimio hilo lisipite kwa sababu ya Urusi ambayo ni mshirika wa karibu wa Iran inayotuhumiwa kuwafadhili waasi hao wa Kishia.

Kwa siku ya 20 ya operesheni ya vita vya dhidi waasi wa Huthi, muungano unoongozwa na Saudi arabia umeongeza mashambulizi dhidi ya ngome za waasi hao.

Jumatatu wiki hii, ndege za kivita za muungano huo, ziliendesha mashambulizi katika Ikulu ya rais Mansour Hadi inayoshikiliwa na wanamgambo wa kishia.

Wakati huohuo mapigano yanaendelea kurindima kwenye mpaka wa Saudi Arabia na Yemen.

Wachambuzi wa siasa za Kimataifa wanabaini kwamba mapigano yanayoendelea nchini Yemen yameendelea kuigawa nchi hiyo.