IRAN-AFGHANISTAN-USHIRIKIANO-USALAMA

Kabul na Tehran zaimarisha ushirikiano dhidi ya ugaidi

Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani yuko Tehran kwa ziara ya siku mbili. Katika ajenda ya mazungumzo na mwenyeji wake Hassan Rohani : kuimarisha ushirikiano katika sekta ya uchumi, nishati na viwanda, lakini pia katika nyanja ya usalama nyanja.

Marais wa Iran Hassan Rohani (kushoto) na Ashraf Ghani wa Afghanistan wakati rais wa Afghanistan alipowasili Tehran, Aprili 19 mwaka 2015.
Marais wa Iran Hassan Rohani (kushoto) na Ashraf Ghani wa Afghanistan wakati rais wa Afghanistan alipowasili Tehran, Aprili 19 mwaka 2015. AFP PHOTO / ATTA KENARE
Matangazo ya kibiashara

Usalama ni suala muhimu kwa Kabul na Tehran dhidi ya ongezeko la ugaidi na itikadi kali za kidini katika katika kanda hiyo.

Kwa siku ya kwanza ya ziara hiyo, marais wa Afghanistan na Iran wamezungumzia suala la ugaidi. Ziara hii inakuja siku moja baada ya mashambulizi ya kujitoa mhanga katika mji wa Jalalabad mashariki mwa Afghanistan, mashambulizi ambayo yaligharimu maisha ya watu 34 na kujeruhi wengine 100. Ni kwa mara ya kwanza mashambulizi makubwa kama haya kudaiwa kutekelezwa na kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu (IS) katika kanda hii inayochukuliwa kama eneo la kihistoria yalikoanzishwa makundi ya Taliban na Al-Qaeda. Ashraf Ghani na Hassan Rohani wametangaza kuimarisha ushirikiano katika mapambano dhidi ya ugaidi, hasa katika maeneo ya mipakani.

Tangu kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu kudhibiti baadhi ya maeneo nchini Syria na Iraq, nchi nyingi zimekua na hofu kushambuliwa na kundi hili, hasa Afghanistan ambayo imeingiliwa sasa na hofu ya kushambuliwa wakati ambapo kikosi cha wanajeshi wa Umoja wa kujihami wa nchi za Magharibi Nato kimekamilisha majukumu yake ya vita dhidi ya makundi yenye silaha hususan Taliban nchini Afghanistan. Zoezi hili la iuimarisha ushirikiano itatokana na mazoezi katika kubadilishana taarifa na kama inahitajika uanzishwaji wa shughuli za pamoja.

Miongoni mwa masuala yanayopewa kipaumbele, marais wawili pia wamejadili tatizo la pamoja: lile la madawa ya kulevya. Iran ni moja ya njia kuu wanakopitia wafanyabiashara wa madawa ya kulevya hadi Mashariki ya Kati na Ulaya pamoja na heroin zinazozalishwa Afghanistan. Tehran imepeindekeza Kabul kuisaidia kupata zao mbadala.