YEMEN-SAUDI ARABIA-HOUTHI-VITA-SIASA

Muungano wa kiarabu watangaza mwisho wa operesheni ya kijeshi

Shawarma mpaka kati ya Saudi Arabia na Yemen.
Shawarma mpaka kati ya Saudi Arabia na Yemen. Clarence Rodriguez/RFI

Muungano wa nchi za kiarabu unaoongozwa na Saudi Arabia katika vita dhidi ya waasi wa Huthi nchini Yemen, umetangaza Jumanne Aprili 21 mwisho wa operesheni yake ya mashambulizi ya anga nchini Yemen, televisheni ya Saudi Arabia Al-Arabia imeeleza.

Matangazo ya kibiashara

Televisheni hiyo imetangaza kwamba muungano huo umeanza operesheni nyingine inayojulikana kwa jina la “ Rejesha matumaini”.

Operesheni iliyojulikana kwa jina la “ Kimbunga chenye maamuzi ” imekamilika, amesema jenerali Ahmed Hasseri,mesmaji wa muungano wanchi za kiarabu unaoongozwa na Saudi Arabia. Muungano huo umebaini kwamba umetokomeza tishio lilikua likizikabili nchi jirani za Yemen. Hata hivyo weng wanaamini kwamba uamzi huo umechukuliwa kutokana na vifo vingi vya raia wa kawaida waliouawa katika mashambulizi ya anga yaliokua yakiendeshwa na muunganohuo. Wakati huohuo Shirika la Afya duniani WHO imetoa ripoti Jumanne wiki hii ambapo imeeleza kuwa watu 944 waliuawa katika mashambulizi ya anga ya muungano wa nchi za kiarabu na wengine 3,487 walijeruhiwa.

Muungano wa nchi za kiarabu ulianzisha operesheni ya kijeshi nchini Yemen Machi 26 mwaka 2015, kwa ombi la rais wa Yemen Abd Rabbo Mansour Hadi, aliye kimbilia Saudi Arabia. Mashambulizi hayo ya anga yaliendeshwa na nchi tisa za kiarabu. Iran imekua ikituhumiwa kuwasadia kijeshi waasi wa Huthi.

Muungano wa nchi za kiarabu una imani kwamba waasi wa Huthi wamepoteza maeneo mengi waliyokua wakiyashikilia.