SYRIA-IS-MAPIGANO-USALAMA

Syria: IS yateka Palmyra

Mji wa kale wa Palmyra, tarehe 14 Machi mwaka 2014. Unesco imeomba Jumatano wiki hii, kusitishwa kwa mapigano ili kuokoa mji huo wa kihistoria.
Mji wa kale wa Palmyra, tarehe 14 Machi mwaka 2014. Unesco imeomba Jumatano wiki hii, kusitishwa kwa mapigano ili kuokoa mji huo wa kihistoria. AFP PHOTO / JOSEPH EID

Wapiganaji wa kijihadi wa Islamic State wameuteka Jumatano wiki hii mji wa kale wa Palmyra, kuashiria kiwango kipya cha kupinga serikali ya Syria na kusababisha wasiwasi kwa ajili ya hazina zake kwa mji huo.

Matangazo ya kibiashara

Udhibiti wa mji wa Palmyra umethibitishwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya ," Syria inayohusika na masuala ya Haki za Binadamu, Rami Abdel Rahman, katika taarifa inayobaini kuondoka kwa wanajeshi katika mji huo wa kihistoria.

Aidha, mwanaharakati mmoja mwenye asili ya Palmyra, Mohamed Hassan al-Homsi, ameliambia shirika la habari la Ufaransa la AFP kuwa Jeshi la Anga limeanzisha kuporomosha makombora yake mjini Palmyra mara baada ya wanamgambo hao kuuteka mji huo.

Katika nchi jirani ya Iraq, wanamgambo hao wameuteka hivi karibuni mji wa Ramadi, mji mkuu wa jimbo la kisunni la Al-Anbar ambapo sasa Marekani wanatathmini mkakati wao nchini Iraq kusaidia serikali kuudhibiti upya mji wa Ramadi.

Kudhibitiwa kwa mji wa Palmyra kunatia wasiwasi kwa vile ni moja ya maeneo muhimu zaidi katika Mashariki ya Kati ambapo siku ya Jumatano Mkurugenzi mkuu wa shirika la umoja wa mataifa linashughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, Irina Bokova ameelezea wasiwasi wake kuhofia kuharibiwa kwa hazina za kale za mji mkongwe wa Palmyra wenye umri wa zaidi ya miaka 2,000.