SYRIA-IS-MAPIGANO-USALAMA

Syria: muungano wa kimataifa washambulia IS

Wapiganaji wa Front al-Nosra, tawi la Al Qaeda nchini Syria, moja ya makundi yanaounda "Jeshi la ushindi" kwenye barabara inayounganisha Aleppo na Latakia, Juni 6 mwaka 2015.
Wapiganaji wa Front al-Nosra, tawi la Al Qaeda nchini Syria, moja ya makundi yanaounda "Jeshi la ushindi" kwenye barabara inayounganisha Aleppo na Latakia, Juni 6 mwaka 2015. REUTERS/Mohamad Bayoush

Kwa mara ya kwanza tangu muungano wa kimataifa unaoongozwa na Marekani kuanza kuendesha mashambulizi dhidi ya Kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu (IS) nchini Syria, mwezi Septemba mwaka 2014, ndege ya muungano huo imefanikiwa kuzuia IS kusonga mbele kaskazini mwa Aleppo dhidi ya wanamgambo wa kiislamu wanoongozwa na Al Qaeda.

Matangazo ya kibiashara

Wiki moja iliyopita kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu liliwatimua wanamgambo wa kundi jingine la kiislamu katika kijiji cha Sourane, kaskazini mwa Aleppo. Islamic State iliendelea na mapigano kwa lengo la kuviteka vijiji vya Mareh na Aazaz. Kudhibitiwa kwa vijiji hivyo kungeliwazuiwa waasi wa Syria kuendelea kupata msaada kutoka Uturuki.

Kutokana na kuendelea kusonga mbele kwa Islamic State, Marekani iliingilia kati na kuwazuia wanamgambo wa kundi hili kutoendelea na mapigano katika maeneo hayo.

Kwa mujibu wa mwandishi wa RFI, katika mji wa Beirut, Paul Khalifeh, mashambulizi manne ya anga yaliyoendeshwa na muungano wa kimataifa dhidi ya Islamic State hayatoshi kwa kuzuia kundi hili kuendelea kusonga mbele, lakini yametoa ujumbe uliyo wazi kwa kundi linaloongozwa na Abou Bakr al-Baghdadi : kuvunjwaa kwa njia kunakopitia misaada ya waasi, ambao wanapigana dhidi ya serikali ya Syria, ni marufuku, hata kama al-Qaeda itafaidika kwa mashambulizi hayo msingi ya migomo haya.

Marekani inafahamu kwamba makundi ya kiislamu katika ukanda huo yanaoongozwa na kundi la Front al-Nosra, ambalo ni tawi la Al Qaeda, ambalo ni moja kati ya makundi yanaunda “Jeshi la Ushindi”, lililoundwa mwezi Machi mwaka 2015, chini ya mwamvuli wa Uturuki, Saudi Arabia na Qatar. Tangu wakati huo, jeshi hilo limekua likipata ushindi dhidi ya jeshi la Bashar Al Assad.