SYRIA-IS-MAPIGANO-USALAMA

Syria: vita vya Tal-abyad, suala la kimkakati kwa IS

Wapiganaji wa Kikurdi katika karibu na mji wa Tal-Abyad,Jumapili Juni 14 mewaka 2015, baada ya kuchukua udhibiti wa mji wa Slok.
Wapiganaji wa Kikurdi katika karibu na mji wa Tal-Abyad,Jumapili Juni 14 mewaka 2015, baada ya kuchukua udhibiti wa mji wa Slok. REUTERS/Rodi Said

Nchini Syria, vikosi vya Wakurdi vimefanikiwa Jumapili mwishoni mwa juma hili lililopita kuingia Tal-Abyad, mji wa Syria uliyo kwenye mpaka na Uturuki, unaodhibitiwa na Islamic State.

Matangazo ya kibiashara

Wapiganaji hao wa Kikurdi wameingia katika mji huo kukabiliana na wapiganaji wa Islamic State, hasa kuudhibiti mji wa Tal-abyad ambao ni muhimu kwa kundi la Islamic State.

Tal-Abyad ni mji ambao unaunganisha mpaka wa Uturuki na mkoa wa Raqqa, makao makuu ya kundi la Islamic State nchini Syria. Kudhibitiwa kwa mji huo na vikosi vya Kikurdi kutawazuia wapiganaji wa Islamic State kuendelea kuingia na kuingiza silaha kutoka nchi za Ulaya au Asia ya Kati na kujiunga na kundi hili la kigaidi.

Kuendelea kusonga mbele kwa wapiganaji wa Kikurdi katika jimbo la hilo kunajibu dhahiri masharti ya kimkakati. Kudhibitiwa kwa Tal-abyad na vikosi vya Kikurdi kutasababisha mji huo kujitenga na mji wa Raqqa, ambao ni makao makuu ya Islamic State nchini Syria. Pia kutapelekea kuhakikisha mwendelezo wa uongozi kati ya ngome ya vikosi vya Kikurdi ya Hasakah kaskazini mashariki mwa Syria, na Aini al-Arab, kaskazini mwa Aleppo.

Wapiganaji wa Kikurdi sasa wapo mita hamsini kutoka Tal-abyad. Vikosi vya Kikurdi vimeendelea kusonga mbele baada ya kuudhibiti mji wa Slok, ambao ni mji mkongwe ambao ni ngome ya zamani sana yakundi la Islamic State nchini Syria. Baadhi vijiji vingine ishirini vilishikiliwa kwa msaada wa ndege za muungano wa kimataifa, ambazo ziliendesha mashambulizi kadhaa yakilengwa katika jimbo hilo.

 

Vita vya Tal-abyad havitakuwa rahisi. Wanajihadi walirudi nyuma katika mji huo, huku wakichimba mitaro, barabara na majengo kadhaa vikibomolewa. Wanajihadi wameimarisha ngome zao katika jimbo hilo. Pia wameharibu madaraja mawili ili kuzuia wapiganaji wa Kikurdi kuendelea kusonga mbele.

Wakimbizi wameruhusiwa kuingia Uturuki, lakini IS inajaribu kuwazuia 

Hatimaye Uturuki imekubali maelfu ya wakimbizi waliokimbia mapigano kuingi nchi humo. Wakimbizi hao walikuwa wakisubiri mpakani kwa muda wa siku nne na ili waweze kuruhusiwa kuingi nchini Uturuki. Jumapili alasiri mwishoni mwa juma hili lililopita, viongozi wa Uturuki hatimaye walikubali kufungua njia, ambapo familia ambazo zilioneka kuchoka ndizo zilianza kuingia, kwa mujibu wa mwandishi wa RFI katika Istanbul, Jérôme Bastion. Baada ya wakimbizi hao kuruhusiwa kuingia nchini Uturuki, wapiganaji wa Islamic State walijaribu kuwazuia raia ili wasiendelei kulitoka jimbo hilo, huku wakiwatishia kwa silaha kurudi nyuma. Labda Islamic State haikutaka watu hao amabo wamekua wakitumiwa kama ngome yao kuweza kutoroka jimbo la Tal-abyad.