SYRIA-IS-MAPIGANO-USALAMA

Syria: mapigano makali katika jimbo la Aïn Issa

Mapigano makali yanaripotiwa katika jimbo la Aïn Issa, karibu na eneo la mpaka la Tall-Abyad, lililodhibitiwa na Wakurdi wiki mbili zilizopita.
Mapigano makali yanaripotiwa katika jimbo la Aïn Issa, karibu na eneo la mpaka la Tall-Abyad, lililodhibitiwa na Wakurdi wiki mbili zilizopita. REUTERS/Rodi Said

Kaskazini mwa Syria, kundi la Islamic State limekua likijaribu kukirejesha kwenye himaya yake kijiji kilichokua chini ya udhibiti wa wapiganaji wa Kikurdi wiki mbili zilizopita, muda mfupi baada ya wapiganaji wa kundi hilo kudhibiti eneo la mpaka wa Tall-abyad.

Matangazo ya kibiashara

Taarifa ya kutekwa kwa jimbo la Aïn Issa hatimaye imekanushwa, lakini ukweli ni kwamba jimbo hilo linakabiliwa na vurugu za mapigano, wakati Uturuki bado inatishia kuingilia kijeshi ili kutenga eneo salama kwa raia wanaokimbia mapigano.

Hata hivyo Kaskazini mwa Syria, kwa sasa, kumekua ni eneo la mapigano. Eneo hilo ambalo limewahi kuwa ngome kuu ya jeshi la serikali limeendelea kushuhudiwa mapigano makali. Awali eneo hilo lilikua likidhibitiwa na kundi la Islamic State, kabla ya wapiganaji wa Kikurdi kulitimua na kuchukua udhibiti wake Juni 24 mwaka huu. Lakini kwa sasa kundi la Islamic State limekua likijaribu kudhibiti eneo hilo. Mapigano yanashuhudiwa hasa kwenye barabara inayoingia katika mji wa Raqqa.

Kwa mujibu wa mwandishi wa RFI Istanbul, Jérôme Bastion, mapigano ya Jumapili mwishoni mwa juma lililopita katika miji ya Aïn Issa, Hassaké ( mashariki mwa Syria) na Sarrin (magharibi mwa nchi hiyo) yamegharimu maisha ya wapiganaji 93 wa kundi la Islamic State. Mji wa Jarablous, eneo la mwisho la kuingilia kwa wapiganaji wa Islamic State kutoka Uturuki, kwenye Mto Euphrate, ulishambuliwa kwa bomu.

Kijiji muhimu cha Sarrin, katika barabara inayounganisha Raqqa na Aleppo, pia kimeendelea kushuhudiwa mapigano makali. Uturuki, ambayo imekua na nia ya kuingilia kijeshi ili kutenga eneo salama ambapo raia wanaokimbia mapigano watalindiwa usalama, imeonywa na Marekani. hata hivyo Uturuki bado inafuatilia kwa karibu jinsi hali inavyoendelea nchini Syria. Lakini Uturuki inapendelea eneo hilo liweze kulindwa na waasi inaounga mkono nchini Syria, kulikua Wakurdi ambao ni inawachukulia kama maadui zake.