Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-TALIBAN-USALAMA

Afghanistan: Mullah Akhtar Mansour, kiongozi mpya wa Taliban

Mullah Akhtar Mohammad Mansour, mpiganaji wa zamani wa Taliban wakati wa sherehe kurasimisha za kuingizwa waasi wa zamani katika jeshi la Afghanistan katika mji wa Herat mwaka 2013.
Mullah Akhtar Mohammad Mansour, mpiganaji wa zamani wa Taliban wakati wa sherehe kurasimisha za kuingizwa waasi wa zamani katika jeshi la Afghanistan katika mji wa Herat mwaka 2013. AFP PHOTO/ Aref Karimi

Baada ya Afghanistan na Pakistan, Twapiganaji wa kundi la Taliban wamethibitisha kifo cha kiongozi wao wa kiroho, Mullah Omar. Wakati huo huo wapiganaji hao wa Taliban wamemteua kiongozi wao mpya: Mullah Akhtar Mohammad Mansour. 

Matangazo ya kibiashara

Lakini kifo cha Mullah Omar kinaweza kuzidisha mgawanyiko ambao umeanza kujitokeza katika kundi la Taliban.

Hayo yanajiri wakati ambapo wapiganaji hao wakitolewa wito wa kushiriki mazungumzo ya amani huku wakikabiliwa na vitisho vya aridhi yao kutekwa na kundi la Islamic State.

Wapiganaji wa Taliban walikua kimya kwa miaka kadhaa kuhusu hatma ya kiongozi wao wa kihistoria, ambaye alionekana hadharani tangu mwaka 2001.

Wapiganaji hao hatimaye wamethibitisha Alhamisi wiki hii kifo cha kiongozi wao. Siku moja kabla, serikali ya Afghanistan ilibaini kwamba mullah Omar alifariki katika " mazingira ya kutatanisha " mwezi Aprili mwaka 2013 katika mji wa Karachi, jirani na Pakistan.

" Uongozi wa Kiislamu wa Emirate (jina rasmi la Taliban) na familia ya Mullah Omar wanatangaza kifo cha mwanzilishi na kifo kiongozi wa Taliban ", wametangaza wapiganaji hao, huku wakitangaza siku tatu za maombolezo na kubaini kwamba kifo cha kiongozi wao kilitokea katika wiki mbili zilizopita.

Wapiganaji waTaliban kutoka afghanistan wamekua wakikabiliwa na ugumu wa kumchagua mrithi wa kiongozi wao wa kihistoria aliye waunganisha kwa miaka 20 na ambaye aliwafikisha madarakani kati ya mwaka 1996 na 2001 kabla ya kutimuliwa na muungano uliokua ukiongozwa na Marekani kufuatia mashambulizi ya Septemba 11 nchini Marekani.

Kwa sasa kumeanxza kushuhudiwa mgawanyiko katika kundi hili la Taliban na huenda kifo cha Mullah Omar kikazidisha mgawanyiko huo ambao umeanza kujitokeza ndani ya kundi hili.

Akhtar Mohammad Mansour, alizaliwa mwaka 1960 katika jimbo la Kandahar, aliteuliwa katikati ya mwaka 2009 naibu mkuu wa Baraza kuu la Taliban, ambalo lina wanachama 10, kabla ya kuteuliwa naibu wa Mullah Omar mwezi Februari mwaka 2010. Akhtar Mohammad Mansour aliwahi kua pia na majukumu katika jeshi la Taliban.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.