PALESTINA-ISRAEL-USALAMA

Cisjordania: baba wa mtoto mchanga aliyechomwa akiwa hai afariki dunia

Watu wakiubeba mwili wa Saad Dawabcheh, baba wa mtoto aliye chomwa moto akiwa hai katika shambulio la moto dhidi ya nyumba yao mwishoni mwa mwezi Julai. Mazishi yake yamefanyika Agosi 8 katika mji wa Duma, nchini Palestina.
Watu wakiubeba mwili wa Saad Dawabcheh, baba wa mtoto aliye chomwa moto akiwa hai katika shambulio la moto dhidi ya nyumba yao mwishoni mwa mwezi Julai. Mazishi yake yamefanyika Agosi 8 katika mji wa Duma, nchini Palestina. AFP/AFP

Mazishi ya Dawabsha Saad yamefanyika Jumamosi hii katika kijiji cha Duma katika ukanda wa Cisjordania.

Matangazo ya kibiashara

Raia huyo wa Palestina alifariki usiku wa Ijumaa kuamkia Jumamosi, Agosti 8, wiki moja baada ya kifo cha mtoto wake mchanga Ali, mwenye umri wa miezi 18, aliye fariki kufuatia shambulio la moto dhidi ya nyumba yao.

Watu wanne wamekamatwa tangu mashambulizi hayo yaliyohusishwa Wayahudi wenye msimamo mkali. Haitoshi, limebaini kundi la Hamas ambalo limetoa wito wa kulipiza kisasi.

Baada ya tukio hilo la moto, Saad Dawabsha alisafirishwa Ijumaa iliyopita akiwa katika hali mbaya katika hospitali ya Beer Sheva, kusini mwa Israeli. Saad Dawabsha alichomwa asilimia 80 na alikua alipoteza fahamu. Madaktari walikuwa walijizuia kuzungumza lolote kuhusu hali yake. Baba wa Ali, mtoto mchanga wa miezi 18, aliye chomwa moto akiwa hai alifariki dunia kufuatia majeraha alioyapata katika shambulio la moto dhidi ya nyumba yake.

Taarifa hii iliotolewa na kiongozi mmoja wa Palestina na kuthibitishwa na ndugu wa marehemu. Mama na kaka wa mtoto mchanga aliyeuawa bado wanalazwa hospitalini, vyanzo vya hospitali vimethibitisha.

kulipiza kisasi

Kundi la Hamas madarakani katika ukanda wa Gaza, limetoa wito leo Jumamosi, katika taarifa yake, wa kusimama kidete dhidi ya uvamizi wa Israel. Vitisho vinavyotia hofu ya kutokea kwa vitendo vya ulipizaji kisase. Alhamisi wiki hii, raia mmoja wa Palestina aliyekua akiendesha gari lake ndogo aliwajeruhi kwa kuwagonga wanajeshi watatu wa Israel katika Ukanda Cisjordania.