UN-SYRIA-MASHAMBULIZI-USALAMA

Syria: UN yachunguza mashambulizi ya kemikali

Je, jeshi la Syria lilitekeleza mashambulizi ya kemikali? Swali ambalo ujumbe wa wataalam unaoundwa na Umoja wa Mataifa unajaribu kujadili. Uamuzi huo umechukuliwa kwa kauli moja Ijumaa wiki hii na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Wanachama 15 wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ikiwa ni pamoja na Urusi,wamepitisha kwa kauli moja azimio la kuchunguza iwapo serikali ya Syria ilitumia silaha za kemikali katika mashambulizi yake dhidi ya waasi.
Wanachama 15 wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ikiwa ni pamoja na Urusi,wamepitisha kwa kauli moja azimio la kuchunguza iwapo serikali ya Syria ilitumia silaha za kemikali katika mashambulizi yake dhidi ya waasi. REUTERS/Lucas Jackson
Matangazo ya kibiashara

Mwafaka huu haukua wa kawaida, kwani Urusi ambaye ni mshirika wa karibu wa utawala wa Syria ni miongoni mwa wanachama kumi na tano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Urusi pia inasisitiza kuwa hakuna ushahidi dhahiri unaoutia hatiani utawala wa Bashar al-Assad.

Ujumbe huo wa wataalam wa Umoja wa Mataifa utaundwa ndani ya siku 20
kuamua kama ndio au hapana utawala wa Bashar al-Assad uliendesha mashambulizi ya kemikali aina ya klorini nchini Syria. Ripoti ya kwanza itatolewa ndani ya miezi mitatu na wataalam kutoka Umoja wa Mataifa na Shirika linalopiga Marufuku silaha za kemikali. Ujumbe huo utadumu mwaka mmoja pamoja na uwezekano wa kuuongezea muda.

Lakini Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameonya kuwa kuna hatari uchunguzi uwe " mgumu " katika nchi inayokaboiliwa na vita. Na hata kama itadhihirika kuwa kuwa serikali ya Syria iliitumia gesi ya klorini kama invyothibitishwa na Marekani, Uingereza na Ufaransa, Urusi, ambayo ni moja wa wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, inaweza kutokuwa na imani na ripoti ya mtaalam au kupinga uamzi wa kuuongezea muda ujumbe wa wataalam wa Umoja wa Mataifa.

Kwa sasa, kupitishwa kwa azimio hili hutoa sura ya umoja kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambalo kawaida limemekua likigawanyika kuhusu machafuko yanayoendekea nchni Syria. Urusi ilizuia maazimio manne ya nchi za magharibi tangu vita vilipoanza nchini Syria. Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa,Samantha Power, amekua na matumaini kwamba, " umoja huo utapelekea kupatikana haraka kwa suluhu la kisiasa ". Tangazo la kuunga mkono mpango mpya wa amani uliopendekezwa na msuluhishi wa Umoja wa Mataifa nchini Syria kwa sasa linajadiliwa katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Kwa mujibu wa balozi wa Urusi, tangazo hili litapitshwa kwa " uwezekano mkubwa " mwanzoni mwa wiki ijayo. Itakuwa ni hati ya kwanza ya kipekee ya kisiasa kupitishwa kwa makubaliano juu ya mgogoro wa Syria.