SYRIA-IS-MAPIGANO-USALAMA

Syria: IS yateka nyara zaidi ya watu 200, ikiwa ni pamoja na Wakristo

Hali ya wasiwasi mkubwa imeendelea kutanda nchini Syria baada ya watu zaidi ya 200 kutekwa nyara katika mji wa al-Qaryatayn, unaopatikana katikati mwa nchi hiyo. Mji huo ulidhibitiwa na wapiganaji wa kijihadi wa kundi la Islamic State (IS), saa 48 zilizopita.

Watu 200, ikiwa ni pamoja na zaidi ya Wakristo 60 wametekwa nyara na wapiganaji wa kundi la Islamic State (IS).
Watu 200, ikiwa ni pamoja na zaidi ya Wakristo 60 wametekwa nyara na wapiganaji wa kundi la Islamic State (IS). AFP/STR
Matangazo ya kibiashara

Tangu kuwasili kwa wapiganaji wa kijihadi, zaidi ya wakaazi 200 wa mji huo walikusanywa na kutekwa nyara. Kwa mujibu wa shirika la haki za binadamu nchini Syria (OSDH), kundi la Islamic State limekua na orodha ya watu wanaotuhumiwa kushirikiana na serikali ya Bashar al-Assad. Baadhi ya watu 170 kutoka jamii ya Wasunni Wakristo 60 ni miongoni mwa wanaotafutwa na kundi la Islamic State.

Askofu mkuu katika mji wa Damascus Mario Zenari, ameelezea wasiwasi wake kwa wakaazi wa mji wa al-Qaryatayn lakini piakwa Wakristo wa vijiji vilio pembezoni mwa mji huo. " Familia nyingi ziliokua zikiishi nje ya mji huo zimekimbilia katika vijiji vinavyokaliwa na Wakristo kama Sadad au Homs ", amethibitisha askofu Mario Zenari. " Tunatarajia kuwa suluhu liko mbioni kupatikana. Ni matumaini yetu na tuendelee kuomba ", ameongeza askofu Zenari.

Nchini Syria, mji wa al-Qaryatayn ulikua na mfano mzuri kwa mshikamano kati ya Wakristo na Waislamu. Katika vita vya wenyewe kwa wenyewe, Mari Elian, kiongozi wa watawa katika mji wa al-Qaryatayn aliwapokea Waislam 700 waliokimbia kutoka Homs. Kabla ya vita mji huo ulikua na Wakristo 2,000. Kwa sasa wanasalia 200 tu baada ya kundi la Islamic State kushambulia mji huo.