SAUDI ARABIA-SYRIA-URUSI-IS-VITA-USALAMA

IS: Saudi Arabia yatupilia mbali wazo la Urusi la muungano na Damascus

Je, kuna njia yoyote ya kuondokana na mogogoro baada ya zaidi ya miaka minne ya vita vinavyoendelea kusababisha vifo vya watu nchini Syria? Hili ni swali ambalo kila mmoja amekua akijiuliza.

Waziri wa mambo ya nje wa Urusi, Sergei Lavrov  (kulia) na mwenzake wa Saudi Arabia Adel al-Jubeir walikutana mjini Moscow. Agosti 11 mwaka 2015.
Waziri wa mambo ya nje wa Urusi, Sergei Lavrov (kulia) na mwenzake wa Saudi Arabia Adel al-Jubeir walikutana mjini Moscow. Agosti 11 mwaka 2015. REUTERS/Maxim Shemetov
Matangazo ya kibiashara

Jitihada za mwisho ni hizi za Urusi, ambayo ilianzisha mwezi Juni, wazo la "muungano" mpya ili kupambana dhidi ya wapiganaji wa kundi la Islamic State.

Baada ya mazungumzo kuhusu suala hilo katika majuma ya hivi karibuni, wazo hilo lilikataliwa na Saudi Arabia kupitia waziri wake wa mambo ya nje, Adel al-Jubeir , ambaye yuko ziarani Urusi tangu Jumanne wiki hii.

Wazo hili lililoanzishwa na rais wa Urusi, Vladimir Putin, mwezi Juni linapania kuunda muungano wa nchi zitakazopambana dhidi ya kundi la Islamic State na shirika dola ya Kiislamu. Urusi imesema, lengo hili la pamoja litapelekea kuzileta pamoja nchi za Saudi Arabia, Uturuki, Iraq, lakini pia serikali ya Syria ya Bashar al-Assad.

Saudi Arabia imsema haiungi mkono mpango huo wa Urusi. Saudi arabia imekumbusha kwamba ni sehemu ya muungano unaopambana dhidi ya kundi la Islamic State, unaoongozwa na Marekani. Saudi arabia imeendelea kusema kuwa Bashar al-Assad ni chanzo cha matatizo nchini Syria na sio suluhu. Kwa upande mwingine, Urusi bado inaunga mkono rasmi utawala wa sasa wa Damascus.

Katika wiki za hivi karibuni, watu wengi waliamini kutokea kwa mabadiliko katika msimamo wa Urusi. Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, mmoja wa viongozi wa kanda anayempinga Bashar al-Assad, alihakikisha siku chache zilizopita kwamba rais wa Syria ameanza kupoteza imani kwa Urusi, jambo ambalo halijathibitishwa hadi sasa na viongozi wa Urusi. Hata hivyo, suala la Syria kwa sasa liko chini ya shughuli za kidiplomasia. Iran, mshirika mwingine wa Bashar al Assad - imehakikisha pia kwamba inaandaa "mpango" kwa mstakabali waSyria.